Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jino la gharama zaidi duniani lina thamani ya dola 36,857. Lilikuwa la mwanamuziki wa zamani John Lennon na lilinunuliwa na daktari wa meno wa Canada Dr Michael Zuk mwaka 2011.
Kabla ya hapo jino la Isaac Newton ndiyo lilikuwa linashikilia rekodi.
Chanzo:Guinness World Records & IndiaToday
 
Sehemu ya nje ya meno ndiyo kitu kigumu zaidi katika mwili wa binadamu. Muundo wa meno yako pia haufanani na muundo wa meno ya watu wengine wote duniani. Hizi ndiyo sababu kuu mbili ambazo madaktari hutumia mabaki ya meno kutambua mtu aliyekufa na mwili wake kuharibika.
Chanzo:NCBI
 
Filamu ya kwanza kabisa kutengenezwa duniani ilikuwa ni Sallie Gardner at the Gallop, ilitengenezwa mwaka 1878, inaonesha tu jamaa akiwa amepanda farasi. Filamu ya kwanza yenye hadithi ilikuwa ni The Story of Kelly Gang, ilitengenezwa mwaka 1906.
KUMBUKA: Televisheni ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1925.
Chanzo:Wikipedia/History of Film, & IMDb
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…