Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Numbisa hizi tafiti nyingine tunatakiwa nasi tujiridhishe hasa kwa hizi zilizokaa ki wepesi.
Nitamtafuata konokono nimtumbue nione ukweli wa meno yake[emoji1787][emoji1787]
Mwaka 2015 wanasayansi waligundua kuwa meno ya konokono inawezekana ndiyo kitu kigumu zaidi cha asili duniani.
Je, Ulijua hili? Konokono anaweza kuwa na meno 14000!
Chanzo:CBS News
 
2016, wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford waligundua kuwa kwenye bonde la ufa nchini Tanzania kuna hifadhi kubwa ya hewa ya helium inayotosha kutumika dunia nzima kwa miaka 14. Majaribio ya uchimbaji yanatarajiwa kuanza mwaka 2020. Helium hutumika kwenye vifaa mbalimbali kama mashine za MRI hospitalini, nishati ya nyuklia kwenye maroketi n.kChanzo:Science Alert, DailyMail, TheCitizen(TZ)
 
Kila wakati wa uchaguzi, tume ya uchaguzi India hutengeneza kituo cha kupigia kura katikati ya msitu wa Gir, Gujarat, ili Mahant Bharatdas Darshandas aweze kupiga kura. Mzee huyo anakaa peke yake huko msituni ambako kuna hekalu. Hivyo kituo hicho cha uchaguzi huwa kina mpiga kura mmoja tu.Chanzo:WeAreIndians
 
Brendan Bremmer, wa Nebraska, US, alijua kusoma akiwa na miezi 18 kwa kujifunza yeye mwenyewe. Alianza chuo akiwa na miaka 11. Lengo lake likiwa ni kuja kuwa daktari wa usingizi (anesthesiologist). Alijiua mwaka 2005 akiwa na miaka 14 ili viungo vya mwili wake vitumike kuwekewa watu wenye uhitaji. Alikuwa mwanamuziki pia.Chanzo:New York Times
 
Mwaka 2011 jeshi la Mexico liligundua shamba kubwa zaidi la bangi nchini humo, pengine na duniani. Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 300 lilikuwa katikati kabisa ya jangwa la Baja. Juu lilikuwa limefunikwa na kitambaa cheusi.Chanzo😀ailyMail
 
Katika jamii ya Tidong, Indonesia, hutaruhusiwa kuuona uso wa bi harusi wako hadi umuimbie nyimbo kadhaa za mapenzi zitakazompendeza wakati wa kufunga ndoa. Pia baada ya ndoa waliooana hawaruhusiwi kuingia bafuni na chooni kwa muda wa siku 3 kuepusha mikosi katika maisha yao.Chanzo:Odditycentral & HuffPost
 
Kabila la Mangaia linachukulia tendo la ndoa kama kitu muhimu sana katika maisha. Wavulana wakifikisha umri wa kubalehe hufanyiwa tohara na kukabidhiwa kwa mwanamke mkubwa ambaye hufanya naye tendo la ndoa ili kumfundisha namna mbalimbali za kufanya kumridhisha mwanamke. Wakishapata elimu ya kutosha, (wote wavulana na wasichana) husisitizwa kuendelea kufanya tendo la ndoa na watu mbalimbali ili kupata uzoefu kabla hawajapata mtu rasmi wa kuishi naye. Baada ya kuoana, wana ruhusa ya kuendelea kufanya tendo la ndoa na watu wengine lakini mara chache ili waweze kuacha baadaye.Chanzo:Sexselvesandsociety
 
Back
Top Bottom