Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WINGI WA WAZEE: Asilimia 23 ya raia wa Italia ni Wazee na kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya nchi hiyo, asilimia 85.6 ya waliofariki kutokana na #Covid_19 walikuwa na miaka zaidi ya 70
-
Ingawa virusi vya #corona vinaweza kuambukizwa kwa watu wa rika lolote, Watu wazee sana ambao kinga yao ya mwili imepungua kutokana na umri, wapo katika hatari ya kuwa mahututi wanapopata maambukizi
 
KUWA NA MAGONJWA MENGINE: Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya Nchini humo (italy), asilimia 48 ya waliopoteza maisha kutokana na #Corona walikuwa na wastani wa magonjwa mengine matatu
-
Taasisi hiyo imesema, "Tuna idadi kubwa ya Wazee wenye magonjwa mengine mengi walioweza kuishi muda mrefu kutokana na kuhudumiwa kwa umakini mkubwa lakini watu hawa ni dhaifu kuliko wengine"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…