Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MACHALE (INTUITION). Ni ile hali au uwezo wa kujua kitu au kukisia jambo, ya bila kuwa na uhakika, uthibitisho au kuwa na sababu thabiti, pasipo kujua ni vipi umepata akili au hisia hizo na sikuzote machale yana ambatana na uwoga. Katika maisha ya kale, machale yalikuwa yana husishwa kiDini na Matendo ya kiroho mfano ,Meditation. Lakini, uhalisia Machale ,ni mawazo ya ndani kabisa (inner feeling au gut feeling), ambayo yana ambatana na ubongo, katika kuchakata taarifa ya bila wewe kujitambua. Machale, ni zawadi ya kila mmoja, lakini wengine wana puuza sanaa yale mawazo ya ndani kabisa. Mfano, utakuta mtu labda unapiga pasi, na unataka kuongeza moto,lakini mawazo yanakujia kwamba nikiongeza moto apa nguo ita ungua, lakini unapuuza unaongeza moto, na kweli nguo inaungua unabaki kujilaumu
 
Machale sikuzote yamekuwa na muungano na mambo mazuri au mabaya, mfano Kifo, ajari, mafanikio, ushindi n.k. Machale sikuzote yana leta majibu kwanza kabla ya tatizo au jambo lenyewe, mfano. unaweza ukawa unapita njia flani,lakini yanakujia mawazo ya kusema kwamba , Nitavamiwa huku mbele, lakini hujui ni vipi utavamiwa na kweli unaweza ukaenda na ukavamiwa kweli na utajua sasa vipengele vyote vya kuvamiwa.
 
Machale yana uwezo wa kukujia ya bila wewe kujitambua, mfano, Unasafari kesho saa kuminambili asubuhi, lakini iyo kesho usingizi ulikushika na ukachelewa safari na gari lina kuacha ,unabaki kulia, lakini baada ya muda kupita unasikia taarifa kuwa lile gari limepata ajari na wote wamekufa, lakini wewe pekeako umepona kwasababu ulichelewa gari. Machale yana uhusiano na maisha ya liyo pita, sasa, na yajayo, kupitia maisha ya kila siku. kwa ujumla kila unacho kifanya ubongo una kihifadhi na sikuzote ubongo una uhusiano na gut feeling (mawazo ya ndani), sasa hisia ikikujia kuhusu tukio fulani ubongo moja kwa moja unalifanya liwe tukio la kweli ambalo, linaenda kutokea iwe ukweli au uwongo
 
Machale yana weza kuwa ukweli au uwongo, na sikuzote ili kuwa karibu na machale yako inakuitaji uwe mtu makini sana katika kuyafuatilia mawazo yako, hisia , ndomana watu wanaojihusisha na mindfulnes , mfano Meditation, wanakuwa na machale sana kwasababu ya umakini wa hisia zao.
 
*WATUMWA WENYE UALBINO.*Ilikuwa ni miaka ya 1920s ambapo ndugu wawili wenye asili ya Afrika, walitekwa na kisha kuzungushwa huku na huko kwenye maonesho mbalimbali na kufanywa kama kivutio cha utalii. Ndugu hao waliojulikana kama *'Muse Brothers'* walizungushwa sehemu mbalimbali za nchi ya marekani, huku wakipewa majina tofauti tofauti kama vile, "watu kutoka sayari ya Mars", "Watu wenye vichwa vya kondoo" na hata wengine waliwaita " watu wanaokula nyama za watu kutoka nchini Ecuador"..
 
800px-Coat_of_arms_of_Pope_Pius_XII.svg.png
 
Majina yao halisi ni George Muse na Willie Muse, ni watoto wa bwana na bibi Muse walioshi katika kitongoji cha Roanoke huko Virginia, Marekani. Babu yao alikuwa ni mtumwa aliyesafirishwa kutoka Afrika na kwenda kufanya kazi kwenye mashamba huko Amerika.
 
Inaelezwa kwamba wakiwa kijijini kwao huko Roanoke, mzungu mmoja aliwateka ndugu hao na kisha kuwapeleka mjini kwenda kuwatumikisha kwenye majumba ya maonesho, ambapo alijipatia kipato kupitia ndugu hao wawili. Baada ya kupelekwa mjini, wazazi walidanganywa kuwa watoto wao (Muse brothers) wamefariki. Hivyo ilikuwa ngumu kurudi tena nyumbani kwao.
 
Wakati wanatekwa, George alikuwa na umri wa miaka 6 wakati Willie akiwa na miaka 9. Walipofika mjini walilazimishwa kufuga nywele 'dreads' kwa lengo la kuwa na muonekano wa tofauti kabisa. Pia walifundishwa kupiga vyombo mbalimbali vya muziki kitu kilicho wavutia watu wengi sana huko Marekani japokuwa walitumikishwa *pasi na kulipwa pesa yeyote* ile, zaidi ya chakula tu ili waendelee kuishi. Mfano, promota mmoja wa maonesho aliyeitwa Al G. Barnes, alizunguka nao huko na huko na hata kufika nchini Canada kwa ajili ya maonesho na asiwalipe kiasi chochote.
 
George Muse na Willie Muse walikuwa wakiuzwa kwa mapromota tofauti tofauti mithili ya watumwa kama watumwa wengine. Lew Graham, meneja wa kampuni kubwa ya 'Ringling Bros. and Barnum & Bailey Circus' aliwatembeza Muse Brothers akiwaita *'Iko na Eko, watu kutoka sayari ya Mars wakutwa kwenye jangwa la California wamedondoka kutoka kwenye chombo chao cha kusafiria".*
 
Bahati nzuri mama yao mzazi, Harriet, alipata kuwaona na kuwatambua wanawe. Akafanikiwa kuwachukua kutoka mikononi mwa kampuni ya Lee Graham. Kisha kufungua kesi mahakamani kuishtaki kampuni hiyo kwa kuiba watoto zake na kuwatumikisha pasi na malipo. Bahati nzuri Harriet alishinda kesi ile na hata kuweza *kulipwa fidia* kutoka kwa kampuni ile.
 
Lakini hiyo haikuweza kuwazuia Muse Brothers kwani waliweza kutoroka nyumbani na kurudi tena kwenye kampuni ya Ringling Bros. and Barnum & Bailey Circus, kuendelea kutumikishwa kwenye maonesho, *lakini safari hii walikuwa wakilipwa.* Walifika hadi nchini Malaysia, lakini pia ulaya kufanya onesho mbele ya malkia wa England. Pesa walizokuwa wakipata waliweza kumjengea mama yao nyumba nzuri ya kuishi.
 
Back
Top Bottom