MACHALE (INTUITION). Ni ile hali au uwezo wa kujua kitu au kukisia jambo, ya bila kuwa na uhakika, uthibitisho au kuwa na sababu thabiti, pasipo kujua ni vipi umepata akili au hisia hizo na sikuzote machale yana ambatana na uwoga. Katika maisha ya kale, machale yalikuwa yana husishwa kiDini na Matendo ya kiroho mfano ,Meditation. Lakini, uhalisia Machale ,ni mawazo ya ndani kabisa (inner feeling au gut feeling), ambayo yana ambatana na ubongo, katika kuchakata taarifa ya bila wewe kujitambua. Machale, ni zawadi ya kila mmoja, lakini wengine wana puuza sanaa yale mawazo ya ndani kabisa. Mfano, utakuta mtu labda unapiga pasi, na unataka kuongeza moto,lakini mawazo yanakujia kwamba nikiongeza moto apa nguo ita ungua, lakini unapuuza unaongeza moto, na kweli nguo inaungua unabaki kujilaumu