Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1585410076025.jpeg
 
Unapaswa kumuondoa mgonjwa nguo zinazobana, bangili ushanga kutegemea na sehemu aliyojeruhiwa. Kama mgonjwa amejeruhiwa mguu mtoe viatu katika mguu uliong’atwa na nyoka. Unashauriwa kumlaza au umkalishe chini ikiwa kama eneo liloathirika ni chini ya moyo. Unapaswa pia kuepuka kumtembeza kwani shughuli yoyote ya kutumia nguvu inaweza kuharakisha mzunguko wa sumu mwilini.
 
Afisa wanyama pori ndugu Lengai anasema Eneo ilioathiriwa/ alilong'atwa/kidonda ama kutemewa sumu unaweza kuosha kwa kutumia maji safi na sabuni. Epuka matibabu ya asili / kienyeji kwani inaweza kumsababishia mgonjwa hatari, njia za asili kama ya kuweka jiwe haina uhalisia wowote wa kuponyesha mgonjwa. Afisa wanyamapori ndugu Lengai anasema mpaka sasa hakuna njia ya asili ya kienyeji iliyothibitishwa na wataalam kuwa inatibu sumu ya nyoka. Inapendekezwa kitaalamu kumsafirisha mgonjwa haraka kwenye kituo cha afya ili aweze kupata huduma za matibabu.
 
Huduma za matibabu hutegemea kama kuongeza maji mwilini ambayo husaidia kuongeza presha ya damu na kupunguza sumu sambamba na dawa za kuua bacteria, dawa za maumivu ikiwa ni pamoja na kuchomwa sindano ya kuzuia tetenasi. Mgonjwa atapewa dawa ya kuondoa sumu mwilini kama ikithibitika nyoka alikuwa na sumu ambayo inaitwa kitaalamu Polyvalent antisera. Mgonjwa na hutakiwa kuondolewa sumu ndani ya dakika 20 la sivyo mgonjwa atafariki. Mtu aliyegongwa na nyoka asiye na sumu hapaswi kupewa dawa ya aina hii.
 
Afisa wanyamapori ndugu Lengai anasema ni vyema kukata nyasi ziwe fupi ndogo na uondoe masalia yote ya nyasi zilizokatwa au majani makavu yaliyoanguka na kujikusanya, kadhalika ni vyema uondoe sehemu za mti zilizoanguka juu ya paa au zinazoning’inia juu ya nyumba yako.Fukia mashimo madogo na makubwa yasiyo na kazi katika maeneo ya nyumbani na mashambani na ondoa vichaka eneo unaloishi.
 
hii ni sumu ambayo inatolewa na nyoka wakati wa kung'ata mtu, asilimia kubwa ya nyoka ambao wapo kwenye mazingira yetu hua hawana sumu yaani kimsingi ukiona mtu ameng'atwa na nyoka leo afu kesho ndio akaenda hospitali baada ya mguu kuvimba basi ujue nyoka yule haukua na sumu.
 
Fukia mashimo madogo na makubwa yasiyo na kazi katika maeneo ya nyumbani na mashambani na ondoa vichaka eneo unaloishi.
dah! hiki chumba ninacholala kimejaaa mashimo.....
kibaya zaidi nalala chini, basi usiku wa leo nimeshuhudia panya wawili wakipiga round kwenye kidoro changu kichafu.

aigoooo Mungu aniepushe na nyoka na sumu yake.
kuna siku nilitafunwa na tandu kwenye makalio (mama weeeee sikupata tena usingizi).

nawatakia mchana mwema wadau wa likes.
 
Mchana mwema pia
dah! hiki chumba ninacholala kimejaaa mashimo.....
kibaya zaidi nalala chini, basi usiku wa leo nimeshuhudia panya wawili wakipiga round kwenye kidoro changu kichafu.

aigoooo Mungu aniepushe na nyoka na sumu yake.
kuna siku nilitafunwa na tandu kwenye makalio (mama weeeee sikupata tena usingizi).

nawatakia mchana mwema wadau wa likes.
 
Back
Top Bottom