Bro samahani nimedandia treni.
Wala sijui chanzo cha hoja zenu.
Ila mwafrika kama hatafika mahali akajitambua kuhusu utu wake na raslimali zake na uchache wa fikra zake.
Na labda ajikubali na ajiamini kwa uchache wa akili alionao mbele ya wenye akili zao, aheshimu vipaji vya watu wake, ubunifu wa watu wake na kujiepusha na vitu vya watu vinavyokuja kama msaada, zawadi au kuomba.
Vinginevyo mwafrika ni binadamu kama walivyo wengine, lakini kosa lake hataki kuishi kwa mujibu wa kanuni zake, mila na taratibu zake.
Angalau tungeamua kuishi kama wanyama wa mwituni.
Yaani tuishi kama tupo kisiwani.
Kwamba tujikubali, kutambua mapungufu yetu na kutafuta njia zilizo ndani yetu kutatua baadhi ya changamoto zinazotukabili.
Vinginevyo tutabaki kuwa watu wa kubezwa, kukanyagwa, kutemewa mate nk.
Sisi bado tunaona ufahari kuomba na wala hatuoni ufaharii kuchapa kazi.
Hata hivyo lazima ujue kuwa mwafrika ni mimi na wewe, tabia hii iliyojengeka baina yetu ya kuwatupia lawama za mara kwa mara viongozi wetu haitatusaidia.
Asante sana