Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

images (18).jpeg
 
Kazi unayo [emoji16][emoji16][emoji16]

Za siku mbili tatu bro? Nyalugusu hapo mnasemaje? Wasukuma wako bado wanakuvunja mbavu na lafudhi yao ngumu wanaongea mpaka mbavu zinawauma?
[emoji16][emoji16][emoji16] tena sio ya kitoto bro

Salama kabsa bro, tupo salama tunaendelea kutekeleza njia za kujikinga na corona,,

habari za huko bro? Familia iko poa?

Wasuku nipo nao hawa[emoji16][emoji16],wazee wa kuoga dak 5 halafu wanaosha yeboyebo nusu saa
 
Bro samahani nimedandia treni.
Wala sijui chanzo cha hoja zenu.
Ila mwafrika kama hatafika mahali akajitambua kuhusu utu wake na raslimali zake na uchache wa fikra zake.
Na labda ajikubali na ajiamini kwa uchache wa akili alionao mbele ya wenye akili zao, aheshimu vipaji vya watu wake, ubunifu wa watu wake na kujiepusha na vitu vya watu vinavyokuja kama msaada, zawadi au kuomba.
Vinginevyo mwafrika ni binadamu kama walivyo wengine, lakini kosa lake hataki kuishi kwa mujibu wa kanuni zake, mila na taratibu zake.
Angalau tungeamua kuishi kama wanyama wa mwituni.
Yaani tuishi kama tupo kisiwani.
Kwamba tujikubali, kutambua mapungufu yetu na kutafuta njia zilizo ndani yetu kutatua baadhi ya changamoto zinazotukabili.

Vinginevyo tutabaki kuwa watu wa kubezwa, kukanyagwa, kutemewa mate nk.
Sisi bado tunaona ufahari kuomba na wala hatuoni ufaharii kuchapa kazi.
Hata hivyo lazima ujue kuwa mwafrika ni mimi na wewe, tabia hii iliyojengeka baina yetu ya kuwatupia lawama za mara kwa mara viongozi wetu haitatusaidia.
Asante sana

Kwani unafikiri Anko wanadanganya basi? Ndio maana ata kipindi kile Trump katupiga madongo watu wa Africa mimi nilikuwa upande wake kabisa

Sema ni vile tu hao Wachina walivyotuongelea ni kama wadudu fulani hatustahili ata kuwepo hapa ulimwenguni [emoji16]
 
Bro samahani nimedandia treni.
Wala sijui chanzo cha hoja zenu.
Ila mwafrika kama hatafika mahali akajitambua kuhusu utu wake na raslimali zake na uchache wa fikra zake.
Na labda ajikubali na ajiamini kwa uchache wa akili alionao mbele ya wenye akili zao, aheshimu vipaji vya watu wake, ubunifu wa watu wake na kujiepusha na vitu vya watu vinavyokuja kama msaada, zawadi au kuomba.
Vinginevyo mwafrika ni binadamu kama walivyo wengine, lakini kosa lake hataki kuishi kwa mujibu wa kanuni zake, mila na taratibu zake.
Angalau tungeamua kuishi kama wanyama wa mwituni.
Yaani tuishi kama tupo kisiwani.
Kwamba tujikubali, kutambua mapungufu yetu na kutafuta njia zilizo ndani yetu kutatua baadhi ya changamoto zinazotukabili.

Vinginevyo tutabaki kuwa watu wa kubezwa, kukanyagwa, kutemewa mate nk.
Sisi bado tunaona ufahari kuomba na wala hatuoni ufaharii kuchapa kazi.
Hata hivyo lazima ujue kuwa mwafrika ni mimi na wewe, tabia hii iliyojengeka baina yetu ya kuwatupia lawama za mara kwa mara viongozi wetu haitatusaidia.
Asante sana



Sent using Jamii Forums mobile app
Daah! Umetisha sana bro 👊👊

Umesema mambo ya msingi na mimi nakuunga mkono asilimia zote kabisa
 
Kwakweli bro Fainali ni lazima ionyeshe utofauti wake na mechi nyingine.
Siyo mnaangalia fainali kama kwamba mnaangalia mechi ya kawaida ya Kombe la mbuzi.
Hebu angalia fainali ya UCL iliyopita.
Yaani unapata goli dakika za mwanzo kisha unapaki basi.
Kabsa bro, fainali za namna ile huwa chache sana..
 
Ndiyo maana nasema tuchukue uamuzi mgumu wa kuangalia tena na tena sera zetu za nje, ikibidi tuji-isolate wenyewe ili tutoke na kitu chetu.
Ni kazi ngumu sana kwenye bara kama hili lilojaa vibaraka wanaodhani huenda na wao ni wazungu ati kwa kuwa tu wamezaa na wazungu, lakini kazi hiyo inawezekana
Mimi Kichina sikifahamu. Nilijaribu kujifunza pamoja na Kiarabu vikanishinda. Ni lugha ngumu ajabu !!!

Comments kama hizi wala hazipaswi kutushtua sana. Popote duniani utakapokwenda mtu mweusi hathaminiwi. Cha ajabu hata yeye mwenyewe hajithamini...Ukitembea tembea huko duniani ndiyo utajua.

Niliwahi kudeti binti wa kizungu siriazi kabisa mpaka akanipeleka kwao kunitambulisha. Ilikuwa familia ya Kikristo sana (wachungaji) lakini kumkubali mtu mweusi iliwawia vigumu mno. Kipindi fulani kwenye kibarua kimoja hivi nikapendekezwa kupewa tuzo ya mfanyakazi bora wa mwaka. Kumbe tuzo hii kwa kawaida wazungu pekee ndiyo huwa wanashinda (inaambatana na substantial $$$). Nilishangaa hata jamaa ambao nilidhani kuwa ni marafiki waligeuka vibaya. Waziwazi kabisa huko wanasema "This award has never been won by a black person and we are not going to change that". Ndipo nikajua kuwa kwa mzungu (na wengineo....) mtu mweusi ni mweusi tu....
 
Back
Top Bottom