Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ankoo hii kesi nije na wakili ama??

Ntakuja jion saizi naingia kupambana na covid kwanza
Corona bebe [emoji137][emoji137][emoji137]
Anko bado nakudai maelekezo... Kule unanikimbia, ushahidi hadi unakaribia kueksipaya [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WASWAHILI wanasema ‘hakuna marefu yasiyokuwa ncha’. Na ‘hakuna milima isiyokuwa na mabonde’. Straika wa FC Barcelona, Lionel Messi anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu kutokana na kipengele kilichopo kwenye mkataba wake na klabu hiyo.
 
Mwaka 2017 viongozi wa Barcelona walionyesha meno 32 nje baada ya Messi kusaini mkataba mpya ambao bila ya kujua ulikuwa ni mkataba unaowapalilia makaa ya moto wao. Kwani mkataba huo ulikuwa na kipengele cha kumruhusu Messi aondoke muda wowote atakapohitaji kufanya hivyo.
 
Kwa sasa viongozi hao wa Barcelona na Lionel Messi wanaonekana kutokuwa na maelewano mazuri, jambo ambalo linaashiria huenda mchezaji huyo asionekane tena klabuni hapo kwa msimu ujao. Messi anaweza akatimkia ikiwa ataondoka Barcelona.
 
MAN CITY

Kama kuna timu ambayo inatamani leo au kesho, kumuona Messi akivaa jezi yake na kuzitumikia nyasi zake ni miamba hii ya pale England. Mara kadhaa Man City ilijaribu kutaka kumsajili lakini Messi alikataa kuondoka Nou Camp. Uwepo wa Pep Guardiola ambaye aliwahi kuwa kocha wa Barcelona na kumfundisha Messi kunachochea zaidi huenda staa huyo wa Kiargentina anaweza akatua kwenye kikosi hicho iwapo atachana na Barcelona.
 
INTER MILAN

Unaweza ukashangaa kuliona jina la wababe hawa wa zamani kwenye orodha ya timu ambazo zinakimbizia saini ya fundi huyu, lakini taarifa zilizotoka mapema wiki iliyopita zinadai Inter Milan nayo pia imeingia kwenye mbio za kuiwania saini ya Messi.
 
Lakini pia hii sio mara ya kwanza kwa Inter kutaka kumsajili mchezaji huyu. Kumbuka kilichojiri mwaka 2006 wakati Messi akiwa na umri wa miaka 18, Inter ilikuwa tayari kulipa kiasi cha Pauni 132 milioni ili kuipata saini yake, lakini Messi hakuwa tayari kuondoka Hispania kwa wakati huo.
 
PSG

Hapa ndo mwisho wa matatizo. Hii ni klabu ambayo viongozi wake hawafikirii mara mbili linapokuja suala la kutoa fedha ili kumsajili mchezaji inayemtaka. Kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi miamba hii ya Ufaransa inatazamiwa kutaka kuwauza washambuliaji wake wawili muhimu ambao ni Neymar anayetakiwa na Barcelona na Kylian Mbappe anayetakiwa na Real Madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…