Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa taarifa yako, Man United, inajivunia dili 61 za matangazo, ambazo ni pamoja na matangazo na kampuni ya mito na godoro na ushirikiano. Yale masuala ya kielektroni na ile ya Denim. Kwa sasa, hakuna ushirikiano na Kampuni za Noodle, baada ya kumalizana na Mamee na Nissin za Japan.
 
United, itapoteza mapato ya Pauni 762 milioni za matangazo ya runinga kama msimu huu wa EPL utafutafutwa kama inavyopendekezwa na wengi. Pamoja na kukosa mapato ya viingilio vya getini ya mechi tano za nyumbani zilizosalia, nne za EPL na moja ya Kombe la Uropa dhidi ya LASK Linz.
 
Lakini hilo wala haliwatishi, kutokana na msingi mzuri wa mapato uliopo klabuni hapo, ndio maana wameahidi kuwalipa vibarua zaidi ya Pauni moja milioni huku pia ikidaiwa iko tayari kurudisha pesa za tiketi kwa mashabiki wao, kama mechi zilizosalia za nyumbani zitalazimika kufutwa kutokana na kusimamishwa kwa ligi.
 
Kama hiyo haitoshi, United pia iliahidi kuwarejeshea mashabiki wao kiasi cha Pauni 245,000 ambazo walilipa katika manunuzi ya tiketi, kwa ajili ya mechi ya ugenini dhidi ya Linz, ambayo ililazimika kuchezwa bila mashabiki.
 
Pia, Mashetani Wekundu, kwa kuonyesha jeuri ya fedha na utu wa kutoa, wameungana na Man City katika kuchangia Pauni 50,000 kila moja, kununua chakula kwa ajili ya jamii zisizojiweza katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na janga la virusi vya corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…