Virutubisho Vinavyoaptikana Katika Machungwa.Machungwa yana mkusanyiko wa virutubisho vingi; Wanga, Protini kwa kiasi kidogo, Vitamini (A, B1,B2,B3,B5,B6,B9, C, E) madini (Kalsiam,Chuma, Zinki,Potasiam) na kambakamba (roughage/fibers).Machungwa ni chanzo kikubwa na kizuri cha Vitamini C katika mlo. Chungwa la ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke. Hivyo chungwa moja au mawili kwa siku yanaweza kutosheleza mahitaji hayo.Machungwa yanaweza kuliwa kama tunda zima au kwa kunywa juisi ya machungwa. Juisi ya machungwa huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi mtu napokula chungwa zima.