Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

credit: ayubu madenge kupitia mtandao wa twitter

Alikuwa mwandishi,Mwanafalsafa,mwanamuziki,mwanadiplomasia,Mwanasiasa na mwanasayansi aliyefanya ugunduzi wa mambo mengi. Benjamin Franklin aliyekuwa mwanachama mzuri wa Freemason ni miongoni mwa ma baba wa taifa la USA.Anaheshimika sana hata akaitwa “The first American”.
 
Wanasema Ben Franklin ni rais ambaye hakuwa rais wa USA. Alikuwa na mchango mkubwa kulipatia uhuru taifa hilo.Alihusika sana kuandaa tangazo la uhuru na katiba ya taifa hilo.Alimiliki watumwa lakini baadaye aliupinga utumwa.Aliamini Mungu yupo japo hakuwa anamuabudu popote.
 
credit: ayubu madenge
Alienda masomoni Ulaya.Aliporudi nchini kwake waafrika wenzake 50 wakauwawa na wakoloni.Akaanzisha harakati za kivita za kuwaondoa Wareno waliokuwepo nchini kwake kwa takribani miaka 500.Mwamba na shujaa wa vita,Amilcar Cabral aliuwawa miezi 8 kabla Guinea-Bissau haijapata uhuru.
 
Cabral alikuwa na uwezo mkubwa kidiplomasia na kivita hata akapewa nafasi UN ya kuzungumza kwa niaba ya wanaofanya harakati wote za kumuondoa mkoloni Afrika. Alishirikiana na viongozi wengine kama Nkurumah na Agustinho Neto katika harakati za kumshinda na kumuondoa mkoloni Afrika
 
Amilcar Cabral alisema uhuru tunaoutaka sio tu wa bendera na wimbo wa taifa bali uhuru wa kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Alipouwawa Kwa kupigwa risasi, Fidel Castro alisema Cabral ni mtu makini aliyewapa matumaini katika mapambano ya kujikomboa.Daima atakumbukwa.
 
Amilcar Cabral alisema uhuru tunaoutaka sio tu wa bendera na wimbo wa taifa bali uhuru wa kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Alipouwawa Kwa kupigwa risasi, Fidel Castro alisema Cabral ni mtu makini aliyewapa matumaini katika mapambano ya kujikomboa.Daima atakumbukwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…