Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UZAZI

Boga pia lina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wanawake ambao wako kwenye umri wa kuzaa(child bearing age) kwani yanasaidia kuchochea uzazi(promotes fertility)Pia Vitamin A inayotokana na beta calotene ni muhimu kwa afya ya mama mjamzito na anaenyonyesha.
 
Utafiti uliofanywa kuhusu zao la korosho, umeonesha kuwa korosho ina faida nyingi sana kiafya, hasa katika magonjwa yenye uhusiano na magonjwa ya moyo, kama ambavyo tutaweza kuona katika makala ya leo, na bila shaka kuanzia leo utaanza kuziangalia korosho kwa jicho tofauti.
 
Kama kweli unajali sana afya ya moyo wako, basi pendelea kula korosho za kila aina. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza (British Journal of Nutrition), umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.
 
Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.
 
Dondoo moja ya ulaji korosho na kujiepusha na magonjwa ya moyo yote mawili (coronary na cardiovascular), inasema kuwa chukua kiganja kimoja cha korosho tafuna au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa β€˜nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki.
 
MADINI YA COPPER, UIMARISHAJI MIFUPA, NISHATI

Licha ya kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Halikadhalika, korosho ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili.
 
KOROSHO NA UZITO

Kuna imani potofu kuwa kwa kuwa korosho ina mafuta, ukipenda kuzila basi mlaji huenda akanenepa. Imani hiyo si ya kweli kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.
 
Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho au butter kwa afya zetu na wala hakuna haja ya kuhofia kuongezeka uzito, badala yaje mlaji ndiye atakaepungua uzito. Elewa kwamba korosho kwa ujumla, ni chanzo kizuri cha madini ya copper, magnesium na phosphorus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…