Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Numbisa kwa Niaba ya wana nyamagana nakuomba ugombee ubunge uwakilishe mawazo ya uzi huu.
Haiwezekani tuwe watazamaji kila siku.
Esta akiingia mjengoni kitanuka. Siku akiamka vibaya hata Spika atakula za uso [emoji16][emoji16][emoji16]

Agombee tuanze kupiga kampeni za chini chini japo jimbo la Nyamagana ni gumu sana halitabiriki (Masha, Wenje....)
 
Awamu hizi zilizofuatana za historia ya Zanzibar zimekuwa na athari kubwa na ya kudumu visiwani. Historia ya utumwa ilikuwa na maana kuwa kila mmoja alionekana, na wengi walijiweka katika makundi ya ama ‘Waarabu’ au waliohusiana na ‘Waarabu’ na waliokuwa wakimiliki watumwa na kwa hivyo Mabwana (mabwana waliokuwa na kila fursa) au Waafrika waliokuwa watumwa waathiriwa wa Mabwana. Hata hivyo, juu ya kuwepo kwa mivutano hii, katika kipindi cha kabla ya ukoloni wa Kiingereza hapajawahi kutokea mgogoro mkubwa wa kikabila.
 
Migawanyiko hii haikuambatana na hali ya kutokuwepo kwa usawa au matabaka katika jamii ya Kizanzibari, hivi sasa au nusu karne iliyopita. Hapo zamani, kama ilivyo hivi sasa, idadi kubwa ya watu ilikuwa ni ya mchanganyiko wa watu wenye asili ya Kiarabu na Kiafrika na makundi ya Waarabu na Waafrika yalikuwa yamechanganyika kiasi kwamba baina ya mwaka 1924 na 1948 asilimia ya wale waliojiainisha kuwa ni Waarabu iliongezeka kutoka asilimia 8.7 hadi kufikia asilimia 16.9 kwasababu wengi ya wale wasiokuwa Waarabu ‘waliamua’ ‘kuungana’ na jamii ya Waarabu’ (Lofchie, 1965: 74), bila ya kuulizwa maswali au kuwekewa pingamizi zozote.
 
Mnamo katikati ya karne ya 20 visiwa hivi havikuwa koloni rasmi bali vilikuwa chini ya himaya ya Uingereza. Lakini nchi zilizokuwa chini ya himaya hazikuwa na tofauti yoyote na zile zilizokuwa makoloni kuhusiana na suala la unyonyaji – Sultani alikuwa mfalme aliye chini ya katiba akilipwa mshahara na Uingereza na wao ndio waliokuwa wakiidhibiti serikali, wakiyadhibiti masoko na njia za kufanyia biashara, na kutia mfukoni faida ya mazao maarufu ya Zanzibar – karafuu na nazi.
 
Wakati huo, mgawanyiko wa kitabaka na kikabila kwa wakazi wa mashamba wa visiwa hivyo viwili ulikuwa ni tofauti kidogo na bila shaka tofauti na ulivyo hivi sasa. Kisiwani Unguja walikuwepo wamiliki mashamba wadogowadogo wasioishi mashambani bali wakiishi zaidi mjini, wakulima wa kilimo cha kujikimu walioishi katika maeneo yasiyokuwa na rutuba nzuri na wavamizi kwenye mashamba makubwa.
 
Katika miaka ya 1950 wamiliki mashamba hawa wa Unguja, takriban wote walikuwa Waarabu. Wakulima wa kilimo cha kujikimu wa Unguja, wengi walikuwa ni Washirazi watu waliochanganya damu, kama alivyo kila mtu Zanzibar, lakini wenye asili ya kutoka Shiraz nchini Iran, ambako wahamiaji kutoka huko waliwasili Zanzibar tokea karne ya 10.

Wavamizi, wengi walikuwa ni watu ambao walikuja kutoka bara ya Tanganyika wakiwa vibarua wa kufanyakazi kwa mkataba wakati wa msimu wa kuchuma karafuu lakini waliendelea kubaki na kuingiliana na wenyeji kwa kuoana, na kwa vizazi kadha wakajumuika katika jamii ya Zanzibar.
 
Hata hivyo, ukabila na matabaka havikuambatana pamoja na wala mfumo wa matabaka haukuwa ni mfumo usiobadilika. Kwa mfano, ijapokuwa Washirazi walikuwa ndio wengi miongoni mwa wakulima wa kilimo cha kujikimu na Waafrika (ambao mara nyingi walikuwa ni wahamiaji kutoka bara) walikuwa ndio wengi miongoni mwa wafanyakazi wa mjini, makabila haya, kama yalivyo makabila mengine, yalikuwa yametawanyika katika mgawanyiko wa matabaka mbalimbali (Kuper, 1970: 366).
 
Namna ambayo ubepari wa kikoloni ulivyoendelea ilikuwa na maana kuwa makabila mengi yalijikuta yakiingizwa, na baadhi ya wakati yakifungika katika kazi maalum na kuwa katika makundi ya kiuchumi ambayo yalikuwa yakikinzana. Kwa mfano, watu wa kutoka Kusini ya Asia waliowasili Zanzibar mapema katika karne ya 1 AD wakiwa wafanya biashara na wachuuzi (Bader, 1991: 170) waliziona shughuli zao za kiuchumi zikipungua mnamo robo ya mwisho wa karne ya 19. Matokeo yake kwa upande mmoja, iliwafanya idadi kubwa ya watu waliotoka Kusini ya Asia waliokuwa matajiri wakaingia katika shughuli za kukopesha pesa. Wakiwa katika shughuli hiyo, waliwatia katika umasikini Waarabu waliomiliki ardhi ambao walikuwa katika hatari iliyosababishwa na kupanda na kushuka kwa bei ya karafuu na hili lilisababisha mvutano kati ya makundi mawili haya
 
Wala sembe walivamia. Wanyamwezi na Wasukuma ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…