Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shinikizo la damu

Unywaji wa pombe hasa kupitiliza umedhibitishwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maradhi ya shinikizo la damu. Imebainikia kuwa pombe huathiri mfumo wa usukumaji wa damu mwilini jambo ambalo hupelekea shinikizo la damu na baadye matatizo mengine kama kushindwa kwa figo, ini n.k.
 
Magonjwa ambukizi

Mara nyingi mtu anapokunywa pombe hupoteza uwezo wa kutawala mwili na maamuzi yake. Hivyo ni rahisi baada ya mtu kunywa pombe akafanya au akajiingiza kwenye matendo hatarishi yanayoweza kumfanya kuambukizwa magonjwa kama vile UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.
 
Ugonjwa wa anemia

Anemia ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kwa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha kwenda kwenye mwili. Hivyo unywaji wa pombe hupunguza uwezo wa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha hivyo kupelekea ugonjwa wa anemia
 
Saratani

Utafiti uliofanywa na daktari Jurgen Rehm, PhD, wa chuo cha Toronto umebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani kutokana na unywaji wa pombe. Utafiti huu ulieleza kuwa tatizo huanza pale ambapo mwili hubadili kilevi (alcohol) kuwa kemikali iitwayo “acetaldehyde”.Saratani huweza kutokea kwenye koo, shingo, mdomo na mapafu. Pia aliongeza kuwa atari inaongezeka pale ambapo mtumiaji wa pombe pia ni mvutaji wa sigara.
 
Kusinyaa kwa ubongo

Kadri umri wa mtu unavyozidi ndivyo na ubongo wake unavyozidi kusinyaa. Hivyo unywaji wa pombe huharakisha kusinyaa kwa ubongo kwa silimia 1.9. Hili hupelekea matatizo yatokanayo na kusinyaa kwa ubongo kama vile kupoteza au kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu.
 
Saratani

Utafiti uliofanywa na daktari Jurgen Rehm, PhD, wa chuo cha Toronto umebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani kutokana na unywaji wa pombe. Utafiti huu ulieleza kuwa tatizo huanza pale ambapo mwili hubadili kilevi (alcohol) kuwa kemikali iitwayo “acetaldehyde”.Saratani huweza kutokea kwenye koo, shingo, mdomo na mapafu. Pia aliongeza kuwa atari inaongezeka pale ambapo mtumiaji wa pombe pia ni mvutaji wa sigara.
Aaah jamani Masanga tena !
 
Msongo wa mawazo

Pombe huathiri mchakato wa kikemikali wa ubongo (Kemia ya ubongo). Kutokana na utafiti uliofanywa, imebainika kuwa watu wanaokunywa pombe nyingi hukabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Msongo wa mawazo ni chanzo cha maradhi mbalimbali kama vile shinikizo la damu, matatizo ya akili, matatizo ya moyo na wakati mwingine kifo.
 
Maumivu ya miguu (gout/jongo)

Gout au jongo ni ugonjwa wa miguu unaotokana na kukusanyika kwa asidi kwenye viungio vya mifupa. Mara nyingi ugonjwa huu hujitokeza sana majira ya baridi. Pamoja na vyanzo vya sababu za kurithi za ugonjwa huu, pombe imedhihirika kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ugonjwa huu.
 
Uharibifu wa mfumo wa fahamu

Hivi leo pombe mbalimbali hutengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali, kemikali hizi kwa kiasi kikubwa huwa na athari kwenye mfumo wa fahamu. Pombe huathiri mifumo na utendeji kazi wa mfumo mzima wa fahamu na kusababisha matatizo kama vile udhaifu wa misuli na matatizo katika milango la fahamu.Hii ndiyo sababu mtu anayekunywa pombe kali anashindwa kuhisi landa za vitu kama vile chumvi au pilipili vyema; hivyo hujikuta akitumia kwa kiasi kikubwa.
 
Kusinyaa kwa uso na macho

Unywaji mkubwa wa pombe husababisha kusinyaa kwa uso na macho hasa kwa wale wanaokunywa usiku. Mara ngingi uwatazamapo wanywaji wakubwa wa pombe utaona hata sura zao zimebadilika na kuonekana zimezeeka au kuchoka kuliko awali.Ni dhahiri umewahi kumwona kijana mlevi wa miaka 25 lakini anaonekana kama mzee wa mika 40. Hii ni kutokana na athari zinazosababishwa na unywaji mkubwa wa pombe.
 
IMG_20200429_221153.jpg
 
Huathiri mifumo ya uzazi

Kumekuwa na mawazo kadha wa kadha kuhusu pombe na maswala ya uzazi. Wengine huamini kuwa pombe huboresha maswala ya uzazi huku wengine wakiamini kuwa pombe huathiri maswala ya uzazi. Ukweli ni kuwa pombe ina madhara kadha wa kadha kwenye maswala ya uzazi kama ifuatavyo:
 
Back
Top Bottom