Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wengi wetu tulipokuwa shule,changamoto kubwa iliyotukabili ni kusoma na kufaulu vizuri mitihani.Tulihangaika kila Siku kujifunza,kusikiliza walimu na hatimaye kumalizi masomo.Kwa hiyo changamoto kubwa ukiwa shule ni jinsi gani utafanya vizuri darasani.Na ndiyo kipimo cha mafanikio yako darasani.
 
Huku mtaani,mafanikio yako hupimwa kwa kutatua changamoto za kimaisha,changamoto zako zinazokukabili unahitaji kuzitatua kwa maamuzi yako.Maamuzi yanaweza kuwa mazuri au mabaya,matokeo ndiyo mafanikio yako.Ukishindwa kutatua changamoto hiyo,uwezekano wa kufanikiwa unaweza kuwa mdogo.
 
Kila hatua ina malengo yake. Hivyo kuanza kwa shule kwa mtoto anaingia moja kwa moja kuwa na malengo ya shule yakiambatana na malengo yake maishani. Malengo maishani ni pamoja na kujua kuwa akiwa mkubwa Siku moja atakuja kuwa mtu fulani maishani. Haya ni malengo!
 
Ndiyo maana,ukimuuliza mwanafunzi Leo anayesoma,tayari anajua kuwa yeye anasoma ili Siku moja aje kuwa mtu fulani. Kwa mfano,kuwa mwanasheria,daktari,mwanajeshi,mwalimu au kuwa mfanyabiashara. Akiuliza sawali hili,unataka kuwa na ni? Utapata majibu hapohapo.
 
Yote haya ni malengo ya utotoni. Baada ya kuhitimu masomo,tofauti na matarajio, huibuka malengo mengine.Malengo ya ukubwani. Katika malengo haya ya ukubwani,yatategemea na malengo ya utotoni. Malengo ya ukubwani huja baada ya kuanza kuona uhalisia wa maisha na kujifunza kutokana na jamii inayomzunguka.
 
Mojawapo ya malengo ya ukubwani,ni kuona kijana au mtu anakuwa huru kifikra,ni kuona mtu anatimiza mahitaji yake ya msingi katika maisha ikiwa ni pamoja na kupata kazi ya kumwingizia kipato,kuwa na familia yake na kujitegemea na kujenga nyumba ya kuishi. Haya ni malengo ya ukubwani.Ni malengo ambaye kila mtu mzima lazima uyafanye.
 
Katika malengo haya,hakuna mtu ambaye atakuuliza tena swali la utotoni katika umri huu. Hutaweza kusikia mtu anakuuliza,unataka kuwa nani? Unataka kufanya nini?. Badala yake,utaulizwa maswali haya zaidi.Umeoa? Una watoto wangapi? Umejenga nyumba? Wengine watakuuza una usafiri?( Gari). Kwa nini hawakuulizi maswali ya utotoni? Ni kwa sababu, muda wake ulishapita. Ushakuwa mkubwa na kwa hiyo unatakiwa kutimiza malengo ya kikubwa.
 
Kila hatua ya ukuaji ina malengo yake. Bahati mbaya sana watu wengi huwa tukifikia katika kimo cha utu uzima ambako kila mtu lazima afanye majumu yake kama mtu mzima hudhani ndiyo ndoto zetu. Kujenga nyumba,kuoa na kuzaa watoto,si ndoto. Ni lazima kwa kila mtu aliyefikia umri huo. Kujitenga na wazazi wako na kuanzisha mji wako ni lazima kwa kila mtu aliyefikia umri wa kujitegemea. Hapa ina maana kuwa huwezi kuanzisha familia ukiwa huna sehemu ya kuishi. Kwa hiyo ujenzi wa nyumba ni lazima.
 
Ukifika umri wa kuitwa mama au baba, watu wanatarajia mambo hayo. Katika umri huo watu hawatakuuliza tena unataka kuwa nani. Badala yake kwa kuwa utotoni ushatoka huko watakuuliza,umeoa?,una nyumba? Una watoto wangapi? Hayo ndiyo mategemeo ya kila mtu aliyetoka utotoni na kuwa mkubwa na kujitegemea.
 
Kwa bahati mbaya sana watu wengi tukifika umri huu,tunajitahidi kutimiza majukumu haya na kushindwa kutoka hapo na kutimiza ndoto kuu za maisha. Wengi tunafikiri kuwa,tukishakuwa na watoto,tukiwa na nyumba za kuishi,tukishakuwa tumeoa na kuolewa basi kazi tumemaliza. Kwamba malengo yetu maishani tumemaliza.
 
Kuoa au kuolewa na kuwa na watoto,kuwa na sehemu ya kuishi na kuwa na gari la kutembelea ni mahitaji ya muhimu kwa mtu mzima. Ni mahitaji ya lazima. Kutimiza mahitaji haya hayategemei kuwa na ndoto kwa mtu. Ndiyo maana,hakuna mtu wa kukuuliza unataka kufanya nini,na kumjibu kuwa,nataka kuwa na watoto au nataka kujenga nyumba. Nyumba,watoto na kuoa ni mahitaji ya msingi kwa binadamu aliyekamilika na mtu mzima.
 
Wengi wetu tumeshindwa kutimiza ndoto zetu maishani kwa kudhani kuwa,tumeshamaliza maono yetu. Ndiyo maana wengi tukifikia umri huu hushindwa kubaini ni kipi tunapaswa kufanya maishani,badala yake tunaishi maisha yetu yote kwa kutimiza majukumu ya lazima kama hayo. Badala ya kushughulika na kutimiza ndoto kuu za maisha yetu tunafika mwisho tukiwa watu wa kawaida tu.
 
ndoto kuu za maisha ni kile ambacho Mungu alikuleta hapa duniani ukifanye. Kila mtu yupo duniani kufanya kazi maalum hapa duniani. Baada ya watu wengi kufikia umri wa utu uzima,wengi wetu hushindwa kubaini ndoto zao. Badala yake anaanzisha familia na kuishi maisha ya kawaida.
 
Ndoto kuu za maisha ni kusudi kuu la maisha yako. Unadhani we we ni nani? Unafikiri watu wanakuona wewe ni nani?Wewe kuishi duniani kutakumbukwa nini ukiondoka?Ukifa Leo watu wakukumbuke kwa lipi? Alama gani utaiacha kuashiria uwepo wako hata ukifa? Majibu ya maswali haya yanalenga zaidi kukuonesha kuwa,kuna kitu unahitaji kukitimiza.
 
Dunia haitakukumbuka eti kwa kuwa ulijenga nyumba. Kama ni nyumba kila mtu anaweza kujenga. Na wengine wanazo nyingi kila sehemu. Jamii haitakukumbuka kwa kuwa ulioa na kuzaa watoto wengi. Kila mtu anao wake na watoto wa kutosha. Tena wengine wanao hata wake wanne. Hakuna mtu atakukumbuka eti ulinunua gari. Kuna watu wengi sana wana magari zaidi yako na ya kutosha.

Ndoto kuu za maisha ni kusudi la maisha yako. Ni jumla ya maisha yako yote. Ndoto kuu ya maisha ndiyo utaifanyia kazi maisha yako yote. Kuitimiza ndoto kuu ya maisha,unapaswa kuifanyia kazi kila Siku mpaka mwisho wa safari yako. Kutimiza ndoto kuu lazima ufanye kwa bidii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…