Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Watu wengi tunaishi bila kujua ndoto zetu. Ndiyo maana wengi wetu tunakuwa wa kawaida. Watu ambao wanatambua ndoto zao katika maisha huanza kuzifanyia kazi wakiwa wadogo na kuzitimiza mapema. Wengine hutambua ndoto zao katika umri mkubwa na hatimaye kuanza kuzitimiza. Ndiyo maana tunashauriwa kujitambua sisi ni akina nani ili tujue mapema na kuanza kuzifanyia kazi.
Ukiangalia watu waliojua ndoto zao duniani,waliweza kufikia mafanikio yao na ni watu wa kukumbukwa mpaka Leo. Ndoto kuu ya maisha inaacha alama( Legacy). Ni utambulisho wa mtu. Ndoto kuu ya maisha inaishi daima hata kama mhusika atafariki Leo,bado ataendelea kuishi kwa kuwa kazi zake zinaonekana. Kila mtu anajua kuwa kile kitu ni cha fulani. Watu wanatambua uwepo wake kwa kazi za kuonekana za maisha yake.Kuna Alama waliacha walipoishi duniani.