Ndoto kuu za maisha yako ni jumla ya maisha yako.Kile unachofanya lazima kikutambulishe duniani. Ukifa Leo,utaacha alama gani!? Nyumba? Gari? Watoto? Mke? Mume? Au utaacha nini? Kama hujawa na ndoto ya kuwa na alama,anza kufikiria upya malengo yako na ndoto kuu ya maisha.
Mpendwa,usiseme, kwa umri ulionao mkubwa huwezi kutimiza. Usiseme kwa umri wako wewe usiseme umechelewa. Ndoto kuu ya maisha haina muda maalum wa kutimia. Kuna watu wengine wanaweza kuziishi ndoto zao na kuzitimiza wakiwa vijana,wengine wakiwa na umri wa kati na wengine wanaweza kutimiza wakiwa wazee. Hii ina maana kuwa kutimiza ndoto kuu ni muda wote wakati bado unaishi. Ni jumla ya maisha yako yote. Kama bado unaishi,bado unao muda wa kutimiza ndoto kuu haijalishi umri wako.
Rafiki,pamoja na majukumu ya lazima katika maisha yako ya kujenga nyumba,kuzaa watoto,kununua gari,bado unahitaji kutimiza ndoto kuu ya maisha. Ni kusudi la maisha yako. Ndiyo utambulisho wako duniani. Ni alama yako. Sasa swali,ndoto yako kuu ni nini duniani?
Ndoto kuu ya maisha ni jumla ya maisha yako yote. Anza kufikiria kuhusu ndoto yako kuu na uanze kuifanyia kazi. Kumbuka,kutimiza ndoto kuu hakuna muda maalum. Hujachelewa na wala hujawahi. Kama bado unaishi,una nafasi ya kutimiza ndoto yako. ” Ndoto kuu ya maisha ni jumla ya maisha yako yote”!
Hata hivyo,kutimiza ndoto kuu,itakubidi ulipe gharama yake!. Si kazi nyepesi,lazima ujitoe na ukubali kusonga mbele,pamoja na changamoto zote hizo, lazima utimize.