Sasa tufanye nini ili tupate yale Mazingaombwe yanayotufurahisha?Kwanza inabidi tutambue umuhimu wa kufanya majaribio (Experiments).Hilo halina mjadala.
Hata simu yako muda wote inaita ndo maana iko hewani.Japo haipigi kelele kwa milio yake, wale walioitengeneza walijuliza maswali tufanye nini ili kelele ya masaa yote inapokuwa on isiwasumbue watumiaji? Majaribio (Experiments) kibao zikafanyika. Nyingi sana zikashindwa na kutupwa kapuni.
Hata mtoto mdogo akishika wembe vibaya utamkata maana hakuna ishara ya kumuonya kama vile ambavyo stovu ya kupikia itamfanya aungue, akimbize mkono na siku nyingine hatarudia tena. Hapo anakuwa amejijengea tabia kwa sababu ya yale maumivu aliyoyapata.
Kwa maana nyingine maisha yako kama ni ya furaha muda wote utaishia kufanya makosa mengi sana maana ile mirejesho ya maumivu ya kukusaidia kujirekebisha inakuwa haipo.
Mazingaombwe ya kugeuza maumivu kuwa furaha inakupasa ujue kusudio lako katika maisha haya. Pia utambue furaha inakutembelea pale unapokuwa umeondoa maumivu ya wengine kwa namna moja au nyingine.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.