Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
MSONGO WA MAWAZO UNAVOSABABISHA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA KIKE NA KULETA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME.Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa. Wanawake wenye PCOS huwa na ovary zilizotanuka na zenye vimbe za majimaji ndani yake. Hedhi isiyokatika au isiyo na mpangilio maalumu, uotaji wa nywele kwa kasi, Kitambi na nyama uzembe, hizi ni dalili ambazo zinaweza kutokea kwa mwanamke mwenye PCOS. Msongo wa mawazo husababisha mwili kutoa vichocheo kama androstenedione ambacho ni kisababishi cha awali cha tatizo cha kujaa majimaji mifuko ya mayai kwa wanawake.