Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ufafanuzi utakaokuja sasa. Ngoja niagize na popukoni kabisa labda tu anko wako asiwe kwenye mudi ya kutoa huo ufafanuzi [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2221][emoji2221][emoji2221]
Mfungo wa jirani zetu lazima tuuheshimu shemeji [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JINSI YA KUPIKA BOFLO MKATE WA ZANZIBAR. MAHITAJI NA VIPIMO. Kipimo cha mikate miwili i. Unga mweupe - 6 vikombe (29 ounces takriban) ii. Hamira - 2 vijiko vya chai iii. Siagi (butter) - 2 Vijiko vya kulia iv. Maji ya dafudafu (warm) - 1 kikombe v. Maziwa dafudafu - 1 kikombe vi. Sukari - 2 Vijiko vya kulia vii. Chumvi - 1 kijiko cha chai NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Weka katika bakuli la mashine (electrical bowl) hamira, maziwa, sukari chumvi na siagi iliyoyaushwa. Changanya vizuri kwa mwiko. 2. Tia unga pole pole huku umeasha mashine ikande, ukiongezea unga mpaka umalizike. 3. Pakaza siagi bakuli jengine kubwa kisha mimina mchanganyiko. Funika kwa kitambaa kilichokuwa kimeloa maji (damp cloth) au karatasi ya plastiki (plastic wrap). Uache unga uumuke mpaka uwe saizi ya mara mbili yake. 4. Utoe hewa unga na umimine juu ya baraza (flat surface). Gawa mchanganyiko sehemu mbili umimine katika treya ya loaf (loaf pan) size ya treya 9 x 5 inchies takriban. Acha uumuke tena kiasi nusu saa. 5. Washa oveni mapema kiasi 200 Degrees uchome (bake) kaisi nusu saa mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown). 6. Epua upoe ukiwa tayari
 
JINSI YA KUPIKA KEKI YA MAZIWA NYUMBANI. MAHITAJI NA VIPIMO i. Siagi - Kikombe 1 ii. Sukari - Kikombe 1 iii. Unga - Vikombe 2 iv. Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe v. Mayai - 4 vi. Baking Powder - 1 Kijiko cha supu vii. Arki rose - kidogo NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki. 2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike. 3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri. 4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose. 5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine) 6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani. 7. Ipike (Bake ) mpaka iwive. 8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.
 
JINSI YA KIPIKA BOGA LA NAZI NYUMBANI. MAHITAJI NA VIPIMO. i. Boga - 1 ii. Tui La Nazi - 2 Vikombe iii. Sukari - 1 kikombe iv. Hiliki - 1/2 kijiko cha chai NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 1. Unamenya maboga kiasi ukipendacho. 2. Unayakata kata vipande vidogo vidogo. 3. Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika. 4. Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki. 5. Kisha unamimina tui la nazi. 6. Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa. Usiwe mchoyo wa Maarifa #SHARE na wenzako wajifunze .
 
MCHICHA SIMPLE WA NAZI: Mahitaji: 🔸Mchicha mafungu 4 🔸Kitunguu maji 1, kilichokatwa katwa 🔸Sukari 1/8 kijiko cha chai 🔸Mafuta ya kula 1/4 kijiko cha chai ,hiari 🔸Tui la nazi zito kikombe 1 1/2 🔸Pilipili mbichi 1 kwa ajili ya harufu ukipenda pasua. NAMNA YA KUTAYARISHA:- 1. Chambua kisha osha vizuri mchicha wako, ukipenda weza ukata roughly kuupunguza kama mkubwa kubwa. 2. Tia katika sufuria pamoja na kitunguu jikoni nyunyiza na chumvi kiasi funika acha mchicha utoe maji. 3. Funua kisha upike hadi upate kukaukia maji (binafsi huwa natia mafuta sasa kisha naukaanga sekunde chache tu 4. Tia tui pamoja na pilipili acha litokote katika moto mdogo hadi lipate kuwa zito. Tayari kwa kula kwa ugali, wali au upendavyo. Note: 🔹Huwa naweka karoti naparua kwa grater pia, ukiweka karoti toa sukari. 🔹Sukari haifanyi mchicha uwe na sukari inasaidia kuboost radha ya mchicha kuwa nzuri zaidi
 
Walishasema picha ndiyo zinawakera zaidi. Maelezo wala hayana madhara. Fafanua pulizi [emoji1545][emoji87][emoji1545]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Naogopa ile "Astakafululahi" yao isije ikanitengua kitendea kazi changu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…