Tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika dunia ya sasa tunayoishi kuna kila aina ya taarifa, matukio na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja katika namna fulani usipokuwa makini yanaweza kuwa moja ya vikwazo vya wewe kushindwa kufanya baadhi ya mambo ambayo ni ya msingi kazini kwako, katika familia yako, katika biashara yako na katika mambo mengine yanayohusu maisha yako kwa ujumla.