Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 78,950
- 236,667
Hivi hadi huko kuna vichaa wengi kama kwingine?Hata kwa Trump huko tunaona. Ukitofautiana naye kidogo tu unatupwa nje. Siasa vs sayansi japo kujifukiza kumekuwepo tangu zamani na tumejifukiza tangia tukiwa watoto....
View attachment 1452221
Kwani yeye alikuwa wapi?Kubishana na wakubwa kuna gharama zake.
Ndugulile alitakiwa kujua kuwa yeye ni mwanasiasa, taaluma yake awaachie wataalam waliopo Wizarani
Ujue wanajichanganya sana.nimeanza kunusa harufu ya movie.....kakutwa na corona bila ya kuonyesha dalili yoyote.
baadae mtakatifu akaziponda mashine za kupima ugonjwa wa covid 19
baada ya wiki mbili mashine zinatuonyesha ya kwamba mama anna kumbe hakuwa mgonjwa wa corona bali ni error
baadae mama anatwambia ametumia dawa za miti shamba
ndani ya wiki mbili amepona corona.
========
kumbe dawa ya kutibu huu ugonjwa tunayo, ya nini kuwasumbua na kuwafedhehesha madereva wa malori ya mipakani
Chief mi kulima sijui naomba nije kukusaidia kuvuna!
Kwani kauli hiyo Ina kosa sehemu gani?Ni protokali mojawapo katika uongozi po pote pale. Huwezi kutoa kauli inayopingana na mkubwa wako hadharani kwa sababu inatoa picha mbaya. Labda kama una ubavu unaweza kutoa dukuduku lako faraghani kama uko tayari kumfunga paka kengele. Ila huko hadharani mbele ya halaiki wote mnatakiwa kuwa na sauti moja. Kama bado hukubaliani na mkuu wako basi unaweza kujiuzulu kuonyesha kutofurahishwa kwako na kutounga mkono suala husika. Huko kwa wenzetu kwenye demokrasia zilizokomaa na wasikotegemea siasa kuendesha maisha yao ndivyo mambo yanavyokwenda. Ndungulile angekuwa ameshaomba kujiuzulu zamani tangu alipotoa kauli hiyo; na mkuu wake ama angemsamehe na kukataa ombi lake au angelikubali lakini mtu unaondoka kwa heshima sana. Watu wasomi halafu matajiri tayari sijui kwa nini wagumu sana kuachia madaraka kwa heshima na kusimamia wanachokiamini. Madaraka matamu sana !!!
Sasa huyu mama alijuaje Kama anayo wakati vipimo wamesema hakuwa nayo kipimo kilikuwa na makosa?Uko deep sana....
Japo kwenye siasa lolote lawezekana lakini huyu mama namwamini sana na sidhani kama anaweza kutumika kwa namna hii. Pengine ni wale wenye immune system nzuri ambao wala hawaonyeshi hata dalili (asymptomatic) mpaka virusi vinapotea.
Kwa hawa madereva wa malori nako kasheshe. Wengine Uganda wanaonekana positive wakifika Kenya wanakuwa negative (and vice versa). Mimi naona kama kuna mchezo fulani unachezwa na hawa viongozi wote wa Afrika Mashariki zikiwemo siasa, pesa za misaada na hata maslahi binafsi.
Naunga mkono hoja ya mwisho.Basi ana bahati mbaya....au tuhitimishe tu kuwa...
Wasukuma siyo watu [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Trump anawalima tweet tu kwamba huna kazi kuanzia leo lakini jamaa unakuta lina net worthy ya milioni 100+ na baadaye inakuja kugundulika kuwa lilishaomba kujiuzulu tangu zamani likakataliwa. Hawa wa kwetu sijui vipi japo kusema kweli hakuna waziri mwenye njaa.
Kuisema serikali vibaya wakati na wewe ulikuwa humo humo ukihondomola miaka nenda miaka rudi ni unafiki tu.
Hujawahi kuusikia kwa Ndodi? Aah nilisahau kumbe we andaeitini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimepata msamiati mpya.
Kuhondomola
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23]
Sijui kwa hapo ila naijua maana ya Dr Ndodi[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio nauona Leo,sijui hata unamaanisha nini
Sent using Jamii Forums mobile app