Mmea huo hukua chini ya ardhi na maua yake ya rangi ya krimu na waridi hukomaa na kuchanua sentimita chache chini ya ardhi.
Ukikasibia sana, mmea huo hufika sentimita mbili chini ya ardhi.
Tofauti na mimea mingine, mmea huu huwa haupati nguvu zake kutoka kwa jua. Badala yake, hutoa virutubisho vyake kutoka kwa kuvu na mimea mingine inayoota karibu. Mmea huu huwa hauna klorofili: kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea ambayo hutumiwa na mimea katika kusanidi nuru na kutengeneza chakula.
Mmea huu huwa adimu sana, na hupatikana maeneo ya Australia Magharibi pekee.