Kwa sababu hukumuweka wazi ni vitu gani unapenda na vitu gani hupendi. Na hatimaye mtaishia kugombana kutokana na kutokuelewana na kutoendana kimahitaji.
2.Jamii Yetu Kuhisi ni Ruksa kwa mwanaume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kutokana na tamaduni mbovu tulizorithi kutoka kwa mababu zetu. Mwanaume anaweza asiwe na tamaa ya kuwa na mpenzi mwingine lakini tu kwa kuona ataonekanaje kwenye jamii anaamua kuwa na mpenzi mwingine.
3. Wanaume wengi hawajui kusema hapana! Ikitokea msichana amekushawishi basi wengi huona hili kama bahati yaani kawaacha wanaume wangapi mpaka kanifuata mimi! Kumbe unajiangamiza.
4 Marafiki wanaomzunguka… Wengi wa wanaume hujikuta wamekuwa na wapenzi wan je kutokana tu na mrafiki anaokaa nao kuwa na tabia hii mbaya! Hivyo humbidi awe na tabia hiyo ili awe sehemu ya kundi hilo.
5. Kudhihirisha UWANAUME wake! Pengine ni kwa imani potofu, marafiki, au tu kwa kumkomoa mpenzi wake, wanaume wengi huamua ku “cheat” kuonyesha tu yeye ni mwanaume wa shoka, na anaweza kufanya lolote, yaani yeye sio “jinsia-mbili”.
7. Familia yake ni watu wa namna hiyo.. hii ni hatari! Kuna wanaume ambao ni wazinzi kwa kuwa tu baba yake, kaka zake, na watu aliolelewa nao wana tabia hii. Ni ngumu sana kumbadili mwanaume huyu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.