Hupunguza uwezo wa kufikili. Wanafunzi wengi wanapopewa maswali ya kufanya shule badala ya kufikiri wao huperuzi kwenye mtandao na hii hudumaza uwezo wa kufikiri.
Hupelekea kuruka chakula. Unapokaa muda mrefu kuperuzi kwenye kompyuta unasahau kula na kujikuta huli kabisa au kula muda usiofaa, hii hupelekea vidonda vya tumbo.
Kompyuta husababisha uvivu na kukosa uwezo wa kufanya kazi zinazohitaji nguvu. Kwa muda mwingi tunaoutumia hutupunguzia uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu Zaidi.
Licha ya Sigara kuwa adui mkubwa wa afya na hata michezo pia, wachezaji wengi wa soka wamekua wakiendeshwa sana na “kilevi” hicho huku wengine ikiwa ni sehemu ya maisha yao! Hapa tumekuandalia list fupi ya baadhi ya wachezaji wanaotumia sigara kupindukia
Wengi wanatarajia kumuona mtukutu huyu kwenye hii orodha, alishawahi kutishiwa na Roberto Mancini kwamba angetimuliwa katika klabu ya man city kwa tabia yake ya kuvuta sana sigara. Pia inasemekana hii ni moja ya sababu ya Mario kuicha klabu yake hiyo ya zamani.
Aligusa vichwa vingi sana vya habari nchini Uingereza baada ya picha yake kusambaa akionekana anavuta sigara kwenye bwawa la kuogelea mwaka 2010. Toka hapo haijawa siri tena kwamba mshambuliaji huyu wa man united ni mtumiaji wa sigara
Kama kuna mtu anagonga vichwa vya habari kwa wingi kutokana na uvutaji wa sigara, basi Ashley cole anaongoza. Huanza kuvuta tu baada ya kupiga mpira wa mwisho kuashiria msimu umeisha. Sigara ndiye rafiki yake wa karibu hasa anapokuwa mapumzikoni
Zinedine ZidaneLicha ya kushiriki kwenye kampeni ya kuzuia uvutaji wa sigara mwaka 2002, Zidanne ameonekana mara kadhaa akipuliza moshi huo hatari kwa afya ya binadamu
Alikumbwa na vikwazo vikubwa baada ya kuonekana akivuta sigara nje ya klabu moja ya usiku na kumuudhi sana meneja wake Arsene Wenger . Japo huyohuyo wenger aliibuka na kumsajili mvutaji mwingine Mesut ozil
Japokuwa yeye hupinga na kudai huweka sigara mdomoni kwa ajili ya utanashat tu, marafiki na wachezaji wenzake mara kadhaa wamekiri kuwa berbatov huvuta sigara kila anapokuwa hayumo kikosini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.