Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Duh!!! Ajabu kubwa
 
Ingekuwa Tanzania watu wangeongea mengi
 
Wanafunzi wote wa Form Six waanze masomo kuanzia tarehe moja mwezi wa 6 kwa zile shule zingine za Sekondari na msingi tujipe muda kidogo, wanachuo ni watu wazima wanajitambua tofauti na mtoto wa darasa la kwanza tujepe muda tuone treds inavyokwenda na wao baadae tutawapa nafasi kadri tutakavyokuwa tunapambana na ugonjwa huu wa Corona" Dkt John Magufuli *KutokaIkuluDodoma
 
MHUBIRI MARTIN BROWN; Wanaosema fedha isikupe kiburi hawajui ni nini maana ya kutafuta fedha , mtu umesota kwa jua na mvua alafu linatokea jitu linakuletea pua yake kutaka kitonga linakwambia braza au sista nipige tafu ya msimbazi wakati kipindi unazisaka walikuwa hawakutambui , unamwambia hapo hapo hamna kumpepesea lugha akakupige tafu baba yako aliye kuzaa , ukizisaka ukipata vimba sana mpaka ardhi ipasuke ,waache waseme hawakuwepo kipindi unatafuta , hii kauli yangu nitaitetea hata mbele za Mungu mbinguni.
 
Mwanamume mwenye umri wa miaka 31, Michael Cook, kutoka eneo la Litherland mjini Liverpool Uingereza, amehukumiwa kifungo cha wiki 12 gerezani baada ya kukiri kuwa amekuwa akimfuatilia mke wake wa zamani kwenye mitandao. Cook alimtumia mpenzi wake wa zamani kwa jumla barua pepe zaidi ya 4,000, alimpigia zaidi ya simu 300 na kumtumia mamia ya ujumbe mfupi ambo mwanamke huyo anadai ulimuathiri kiakili. Kulingana na mwanamke huyo Bw Cook alikuwa anamtumia ujumbe wa vitisho kuwa angejiua mara kwa mara na alitumia njia mbalimbali mfano aliwatumia ujumbe watu wa familia yake, wapenzi wake na marafiki hata wafanyakazi wenzake kazini. Mwanamke huyo aliamua kumshtaki mwanamume huyo ili mwanamke yeyote au mwanaume ambaye anapitia maisha sawa na yake kujua kuwa hii si sawa na kwamba lazima atafute usaidizi. Mahakama imemwamuru Cook kutowasiliana na mpenzi wake wa zamani kwa miaka mitano.
 
Watoto wachanga 50 waliozaliwa kupitia mpango wa kukodi kinamama kubeba ujauzito kwa niaba ya wazazi wao wamekwama katika hoteli moja ya Kyiv Ukraine 🇺🇦. . . Katika harakati za kupambana na ugonjwa wa Corona,Ukraine ilifunga mipaka yake ila kwa shughuli za dharura. . . Wazazi wa watoto hao wanaotoka kote duniani kuanzia China Argentina Italia na hata Argentina wameshindwa kusafiri kupokea malaika hawa. . . Wengi wanakabiliwa na changamoto za uzazi na hivyo kuamua kukodi wanawake Ukraine kwa takriban dola $50,000. Biashara Hii ni halali nchini Ukraine. Je kwanini wazazi wao wasiruhusiwe kuwapokea hawa malaika wa Mungu? Je hii si shughuli ya dharura baada ya kumtafuta mtoto kwa miaka ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…