Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

maisha na changamoto tambua Bila ubunifu biashara yako inaweza kuporomoka na pengine kufa kabisa .
 
Ili kuwa mbunifu ni vema kuacha mazoea na kuanza kujaribu mawazo chanya mapya kwenye biashara yako.
 
Faida hizo za ubunifu katika biashara ni1.Kuboresha Biashara.Ubunifu katika biashara yako utafanya bidhaa au huduma unayoitoa kuwa na viwango vya hali ya juu na kupelekea biashara yako kuwa yenye thamani sokoni.Nakuoneka na kuwa ya kipekee katika eneo husika.
 
2.Kufanya uwe wa kipekee.Ukiwa mbunifu katika biashara yako, ubunifu utakutenga na kuwa mtu wa tofauti hata kama mnatoa bidhaa au huduma zinazofanana,mfano saluni zetu kuna wale wanaotoa huduma za kawaida ambao haweki maji ya moto au vuguvugu kwa ajili ya kumsafisha mteja akisha nyolewa.hawa watakuwa tofauti na wanao tumia maji ya moto au vuguvugu,Acha mazoe fanya kipekee.
 
3.Kufikia wateja wengiIli uwafikie wateja wengi ni lazima kuwa mbunifu katika bidhaa au Huduma unayoitoa,fanya kuwa watofauti acha mazoea utateka watu wengi katika soko lako.kuwafikia wateja wengi ni faida ya ubunifu katika biashara yako.
 
4.Ujasiri katika BiasharaUnapotoa huduma bora na kuuza bidhaa zenye viwango vya hali ya juu ni lazima utajiamini maana wewe ni wa kipekee,na huduma au bidhaa zako ni za viwango vya juu.
 
ILI UFANIKIWE NI LAZIMA UWE MSIKILIZAJI MZURI(Be a good listener)Kufanikiwa. Unatakiwa kujifunza ni jinsi gani?usikilize kwanza,kuwa msikilizaji ni mafunzo ambayo yatakujengea tabia ya kifanya kitu au vitu kwa umakini maana umepokea kile unatarajia kukifanya,
 
Weka umakini mkubwa na kuwafuatilia watu wenye mafanikio makubwa katika na sha yako na kufanya kwako hivyo utakuwa unaiona njia ya mafanikio yako
 
Hudhuria semina ,warsha,makongamano mbalimbali yanayo hubiri njia au mbinu mbalimbali za kuukimbia umaskini pitia kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook,youtube,tweeter,instagram,n.k sikiliza wahamasishaji,walimu,wabobezi wa nyanja mbalimbali juu ya kutoka kimaisha na kulikimbia wimbi la umasikini.
 
ACHA KULALAMIKA(Stop the complaining)Unaweza kufikiri ya kwamba hakuna uhusiano kati ya kulalamika na mafanikio yako ya sasa.Ukweli ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitu hivyo viwili katika maisha yako.
 
Tambua unapoteza muda mwingi sana katika mambo yasiyokuwa na faida ukizidi kulalamikia hayo mambo na pia utakuwa unaua mtandao wa mafanikio yako kwani umejaa lawama tuu
 
Badala ya kufikiri changamoto hizo kama ni tatizo bali fikiri kama fursa ,Ukifanya hivyo utafanikiwa na utawasaidia watu wengi sana na utakuwa umeukomboa wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…