Husaidia seli na tishu mwilini kwa vitamini c iliyomo katika tunda hili suala linalopelekea kujengwa kwa sehemu muhimu ya protini iitwayo COLLAGEN ambayo huimarisha mishipa ya damu,ulinzi wa ngozi,ogani na mifupa mwilini.
Nanasi ni tunda lenye faida kubwa sana mwilini mwako hizo ni chache kati ya nyingi, hivyo tumia fursa ya gharama ndogo ya matunda haya kwa faida ya afya yako.
Huuzwa nchi nzima kwa bei ndogo na ya kawaida kabisa huku likiwa na faida kubwa sana kiafya.Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye tunda hili ni;Vitamini K __________ 26%Folate __________ 20%Vitamini C __________ 17%Potassium __________ 14%Vitamin E __________ 14%Vitamin B5 __________ 14%Vitamin B6 __________ 13%
Kwa orodha ya virutubisho hivyo hapo juu Parachichi litasaidia sana mwili wako kurekebisha msukumo wa damu, Tunda hili lina 77% ya protini kitu kinachofanya tunda hili liwe mmea wenye protini kuliko mwingine wowote ule.
Papai ni moja ya tunda zuri,tamu likiwa vilevile linapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Kama ulikuwa hujui faida za papai kwa afya yako ngoja nikuibie siri.
Papai ndio tunda lenye utajiri wa madini mengi sana ukilinganisha na matunda mengine pamoja na virutubisho vingine vingi.Baadhi ya faida za tunda hili ni kama vile;.
Husaidia sana kupunguza uzito (weight loss), Ikiwa kila nusu kipande kikiwa na Calories 120.Tunda hili ni la muhimu sana kwenye suala la kupunguza uzito β¦kama unashida ya uzito usiotakiwa tumia tunda hili mara kwa mara litakusaidia sana.
Husaidia sana kinga ya mwili kwa zaidi ya 200%.Utajiri wa Vitamini C papai lililonao husaidia kinga ya mwili kuwa imara pindi unapotumia mara kwa mara.