Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nimeiangalia hii picha kwa jicho lingine kabisa...

Wanadamu tukubali kuwa si kila tatizo tulilo nalo ni la kulitatua, yapo mengine ni kwa ajili ya kutujenga kiimani na kutuheshimisha kwenye jamii, ikitokea binadamu huyo akaondoka duniani akiwa kwenye mapambano ya kutatua matatizo yasiyo tatulika kiasili, basi, ndugu na jamaa watamlilia na kumsifia kwa upambanaji wake pasi kuchoka hadi umauti kumfika.

Matatizo mengi yasiyo tatulika huwa hayajifichi, tumebeba mizigo vichwani mwetu, mikono yetu uhangaika kutafuta suluhisho, ni mizigo/matatizo ya asili,tutakufa nayo, tutaitwa MASHUJAA kwa kuipambania familia/jamii iliyo tuzunguka...
Tusichoke kujihangaisha kuzitatua changamoto zetu maana hatuzijui ni zipi zina tatulika na zipi ni za asili...

Natamani siku yangu ikifika ya kuondoka hapa duniani,basi, mizigo hii iwe moja ya sababu ya familia/jamii yangu kunililia na kunikumbuka katika maisha yao.

TUKIPATACHO TUGAWANE NA WENZETU WASIO JIWEZA [emoji120][emoji120]View attachment 1461594
Leo umekuja kivingine kabisa. Kwa falsafa hii chanya kuhusu maisha hata Plato na Aristoto wakasome. Nikiongeza kitu nitaharibu...

Na leo sisomi kitu tena. Hii inatosha. Ni kuicheua tu na kuitafakari. Mungu na Akatusaidie [emoji1545][emoji1545]
 
1. Mwanaume huzalisha mbegu milioni kumi za uzazi siku! Kwa maana hiyo, anauwezo wa kujaza idadi yote ya dunia kwa miezi sita tu!
Jizazi
20200528_113425.jpg
 
Back
Top Bottom