Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiungo wa Atletico Madrid na mchezaji anayefikiriwa pia na Manchester United Saul Niguez amesema atatangaza ''klabu mpya'' ndani ya siku tatu zijazo. Raia huyo wa Uhispania, 25, mkataba wake na timu ukitaka kuweka mezani kitita cha pauni milioni 130 ili kumnyakua .(Manchester Evening News)
 
Inter Milan wamesema kuwa wanataka kuendelea kumshikilia mshambuliaji wa Manchester United Alexis sanchez kwa mkopo baada ya tarehe 30 mwezi Juni. Mchezaji huyo anaichezea klabu hiyo ya ligi ya Serie A mpaka mwishoni mwa msimu. (Sky Sports Italia)
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya FIFA, Pierluigi Collina katika barua yake kwa vyama na mashirikisho ya soka, amesema kuwa kamati hiyo haina mamlaka ya moja kwa moja juu ya adhabu kutokana na kosa hilo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa hivi karibuni.
 
Kumtemea mtu mate ni kosa la kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa mujibu wa sheria 17 za soka. Hata hivyo utemaji mate unapokuwa haujaangukia katika namna hiyo, ni vigumu utekelezaji wa kutoa kadi ya njano kwa refa kwa sababu unaweza kutokea kokote ndani ya uwanja.
 
Kutokana na hilo mashindano yanapotoka kuweka protokali juu ya utemaji mate, uamuzi wowote wa kinidhamu unatakiwa kutolewa baada ya mechi na waandaaji wa mashindano, chama au shirikisho la soka la nchi husika," ilisema barua hiyo ya Collina.
 
Ligi mbalimbali zimeanza kurejea duniani baada ya kusimama tangu mwezi Machi, k ikiwa ni miongoni mwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na virusi vya Corna ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Covid19 unaoweza kuwa chanzo cha homa kali ya mapafu.
 
Man United chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer inatarajia kuwa bize wakati dirisha lijalo la usajili litakapofunguliwa licha ya kuripotiwa kuwapo kwa hali ngumu ya kiuchumi kutokana na janga la corona, ambalo limeziathiri klabu nyingi za soka.
 
Kwa mujibu wa ESPN, Sancho bado anapewa kipaumbele kikubwa cha kunaswa na mabingwa hao mara 20 wa England, lakini wakali wengine Jack Grealish wa Aston Villa, Moussa Dembele wa Olympique Lyon na Timo Werner wa RB Leipzig ni washambuliaji waliopo kwenye orodha ya wanaowindwa kwa udi na uvumba huko Old Trafford.
 
Mastaa Grealish na Dembele nao wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kuzihama timu zao, Aston Villa na Lyon mtawalia kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, huku Werner naye maisha yake yamekuwa yakiandamwa na uvumi wa aina hiyo siku za karibuni.
 
Liverpool wamekuwa wakihusishwa sana na kutaka saini ya straika huyo wa RB Leipzig, lakini imeelezwa kwamba janga la corona limetikisa timu nyingi kiuchumi na jambo hilo linaweza kuwabana wakali hao wa Anfield wakashindwa kuwa na pesa inayotosha kunasa huduma ya Mjerumani huyo aje kwenye timu yake kwa ajili ya msimu ujao wa 2020-21.
 
Back
Top Bottom