Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 1960 Vicky na mwanamuziki mwingine aliyejulikana kwa jina la Brazzos walijiunga na Josepph Kabasele ‘Grand Kale’ pamoja na wasanii wengine wa bendi ya African Jazz ambayo ilikuwa bendi hasimu na ile ya T.P.OK. Jazz, wakaenda kushiriki kurekodi kwenye maonesho ya kurekodi jijini Brussels nchini Ubelgiji.
 
Vicky alichangia kwa kisai kikubwa katika wimbo wa Joseph Kabasele unaoitwwa ‘Independence Cha Cha’ ulikuwa mmoja wimbo ulipata umaarufu mkubwa kuliko zote nchini humo.Alitunga nyimbo nyingine zilikiwemo za ‘Vive Lumumba Patrice’ na‘Sentiment Emonani’.
 
Kuondoka kwake kwenda Ubelgiji, kuliharibu uhusiano waka na bendi ya T.P.OK. Jazz hata alivyorejea kutoka huko aliungana na Dihunga ‘Djeskain’ Armando Brazzos aliyekuwa ametoka bendi ya T.P.OK Jazz, Johnny Pinnock na Leon Bholen Bombolo wakaunda bendi yao mpya waaiita Negro Success.
 
Alipokubaliwa kurudi T.P.OK.Jazz aliendelea kuchangia katika uimbaji akiwa ‘back vocal’ kando ya Franco na Edo katika vibao vilivyoweza kushika chati vya ‘Ngai Marie Nzoto Ebeba’ ikiwa na maana ya Yaani mimi Marie ambaye mwili wangu unakwisha’, ambao ilikuwa ni hadithi ya kahaba wa Kinsahasa.
 
Vicky aliandika nyimbo nyingi akiwa na bendi ya T.P.OK. Jazz zikiwamo za ‘Conseil d’Ami’ ikiwa na maana ya ‘ushauri wa rafiki’ uliopigwa katika mtindo wa polepole wanye ladha ya ‘bolero’ uliokuwa unapendwa sana na Vicky Longomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…