Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1586759569045.jpeg
 
Tukio la kumpokea yule kibopa, tena kuja kugombea urais, tena kumpa nafasi hiyo bila hata kupitia mchakato wa kidemokrasia lilikuwa kosa kubwa la kiufundi ambalo ilipaswa kuondoka kwa safu yote ya kamati kuu kistaraabu ili waanze upya. (Walitakiwa wajiuzulu kwa hiyari)
Ila cha kushangaza ndani ya chama hicho hakuna anayejali usanii huu mbele ya macho ya wapiga kura wasio na vyama ambao mara nyingi ndiyo wanaoamua mshindi
Kupiganiwa sawa lakini pia na mpiganiaji awe na haiba na matakwa yanayoeleweka. Na mpiganiwaji ajue kweli kuwa yumo matatizoni na anahitaji kupiganiwa. About turn ya 2015 ina gharama kubwa mno na mpaka watakaporudi kwenye upya wa sera za kikombozi walizoanza nazo na kuachana na hizi siasa za mazingaombwe, matukio na kutafuta huruma ya umma kwa gharama yo yote ile, itawachukua muda sana nao kukaa kwenye viti vya mbele kwenye meza ya mfalme ili kufakamia keki ya taifa. Wakiri kuwa lilikuwa ni kosa la kimkakati kumkaribisha yule mzee na sasa wamerudi kwenye sera komavu endelevu. Natamani wafanye hivyo kabla hawajaingia kwenye uchaguzi wa mwaka huu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom