Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ali karume amechukua tena fomu, haiba yake ya uongozi si njema sana (nafasi ya uraisi nayo ina mvuto wake mbele ya hadhira).
mfumo wake wa Maisha nao pia ni sintofahamu (sina uhakika kwa sababu sijawahi kwenda viwanja vya wanywaji, ila jamaa inasemekana ni mpenda sana maji ya kiwandani),
mbwatukaji (kesho atasifia muungano, kesho kutwa ataponda muungano)
 
Aisee...Ana chembe chembe za uanaharakati kama shangazi wa taifa?...

Watachaguana wenyewe humo humo kwenye system yao...

Maalim Seif bado ana ushawishi hasa huko kwao Pemba? Natamani agombee kwa mara ya mwisho awatingishe tena japo siamini kama atawatingisha kama alivyofanya 2015. Wengi wanaamini alishinda.

Imagine kuukosa urais ulioupigania miaka na miaka...na ukashinda ila tu system ikawa haikutaki. Inauma ila kwenye heka heka za kisiasa kila jambo linawezekana...

Cha muhimu tu tuwe na uchaguzi wa amani.
 
Maalim Seif bado ana ushawishi hasa huko kwao Pemba? Natamani agombee kwa mara ya mwisho awatingishe tena japo siamini kama atawatingisha kama alivyofanya 2015. Wengi wanaamini alishinda.
maalim alishinda kweli (ccm walifanya makosa uchaguzi ule, kujiamini kwao kuliwatokea puani kwani waliruhusu kila chama wajumlishe kura zao za uraisi kupitia vituo vya kupigia kura)

zamani kura za uraisi zilikuwa zinahesabiwa kwa pamoja na majumuisho ya matokeo yanafanywa na tume.
hapo ndipo walipofanyiwa suprise ya mwaka, jamaa walipoamka asubuhi wakatangaza jumla ya kura walizopata za uraisi kupitia kituo chao cha habari kinachoitwa swahiba Fm (mwaka 2015 cuf walijipanga kwa kila kitu kuanzia bajeti ya kampeni mpaka wataalamu wa IT)
 
Imagine kuukosa urais ulioupigania miaka na miaka...na ukashinda ila tu system ikawa haikutaki. Inauma ila kwenye heka heka za kisiasa kila jambo linawezekana...
Jamaa ni mwepesi wa kuridhia, kwa mujibu wa mzee nassor moyo anasema ya kwamba hata uchaguzi wa mwaka 2010 maalim seif alimshinda kwa kura dokta shein......

kilichofanyika ni maridhiano ya kisiasa lakini kwa sharti kuu:
no compromise uchaguzi wa 2015

picha : miaka 10 iliopita baada ya shein kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi ukumbi wa bwawani


Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa Zanzibar 2010 | DW | 23.10.2014
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…