myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Alikabiliwa na mateso ya kisaikolojia na kudhalilishwa kabla ya kusafirishwa na kupelekwa Afghanistan katika hali ya kutisha. Akiwa Afghanistan alizuiliwa katika magereza matatu ya Shirika la Kijasusi la Marekani pamoja na lile ovu maarufu ‘Gereza la Kiza’ na lile la ‘Shimo la Chumvi’. Kiasi cha mwaka mmoja baadae, alisafirishwa kwa ndege hadi Tunisia ambako aliwekwa kizuizini kwa siku 75 nyengine kabla ya kurudishwa Algeria ambako aliachiwa huru.
AiseeKwa mfano, balozi wa Marekani Mark Green mwezi Februari 2008 aliandika katika ‘maelezo mapya kuhusu suala la ugaidi Tanzania.
Kuanzishwa kwa Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi Tanzania ni suala la kipaumbele kwa Tanzania … Hata hivyo, mipango na muda wa kiutekelezaji wa kituo hicho vinaendelea taratibu sana kwasababu ya ukosefu wa fedha. Ili kuongeza uelewa wa Serikali ya Tanzania juu ya faida za Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi, mwezi Oktoba 2007 Ofisi ya Mratibu wa Vita dhidi ya Ugaidi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, 2001-09) iligharamia safari ya afisa mmoja wa [Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania] kitengo cha kupambana na ugaidi na afisa mmoja wa Kitengo cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Polisi la Taifa ili kukitembelea Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi cha Yemen mjini Sanaa. Kutokana na ziara hii, maafisa wote wawili wametambua juu ya ulazima wa kukikamilisha Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi cha Tanzania, na kuajiri watumishi wake kikamilifu. Hata hivyo, uhaba wa fedha bado umebakia kuwa ni kizingiti. (Ubalozi wa Marekani, 2008c)
Aisee..Tarehe 4 Februari, kwa mara nyengine tena Lenhardt amekuwa na habari njema kwa Marekani. Safari hii ni kuhusu Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambalo tokea kuteuliwa kwa mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange mwaka 2007 amekuwa ‘akiboresha vifaa vya kijeshi vilivyochakaa vya jeshi hilo na kujihusisha zaidi na masuala ya kikanda na shughuli za kimataifa za kulinda amani na amekuwa karibu na jeshi la Marekani.
Duh!!!Kama ilivyofichua WikiLeaks, Marekani ina hamu ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Tanzania itakayoijumuisha CUF. Hii si kama itawanyanyua viongozi wa sasa tu, kuondoa uwezekano wa kuwa na vijana wenye siasa kali na kuleta ‘utulivu’, bali serikali kama hiyo vile vile itakuwa na fursa ya kuiwezesha Marekani kushirikiana na viongozi na wafuasi wa CUF.
Kwa mujibu wa mtoaji habari mwengine, Dk. Ndumbaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na rafiki mkubwa wa Dk. Mukandala kwenye REDET, ni rahisi kufanyakazi pamoja na wanachama wa CUF ‘kwani CCM bado inalazimika kutengeneza mazingira mazuri ili sekta binafsi istawi … wafanyabiashara wengi na wachuuzi ni wafuasi wakubwa wa CUF’.
Huyo mtoto ni wa kike au kiume?
Wa kiumeHuyo mtoto ni wa kike au kiume?
Aisee....kaazi kweli kweli.Wa kiume