Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unajua kilitokea nini?Ni wakati huo wa Tauni "Babonic Plague", Newton alishuhudia Tufaa(Apple) likianguka toka mtini kwenye bustani ya familia huko Woolsthorpe(Maili 50 hivi toka Cambridge). Hapo alijiuliza maswali yaliyopelekea Ugunduzi wa Nadharia ya Nguvu ya Uvutano(Gravity).Newton alifanya Majaribio kadhaa ya Mwanga pia yaliyopelekea kuandaa Nadharia za Optiki.Haitoshi, Newton aliandaa njia na kanuni mpya katika fani ya Hisabati. Zikawa chimbuko la Calculus!Robo ya Wakazi wa London walifariki kutokana na Tauni kati ya 1665 na 1666.
 
Newton alirudi Chuoni Cambridge mwaka 1667, akiwa na nadharia alizoziandaa akiwa nyumbani. Ndani ya miezi 6 tu, alifanywa kuwa mtafiti(Research Fellow) na miaka miwili alitunukiwa Uprofesa Chuo Kikuu Cambridge.
 
Nakujuza!Washabiki waliovaa barakoa wakifuatilia mechi ya nyumbani ya timu ya Georgia Tech kwenye ligi, maarufu "College League" mwaka 1918. Ni wakati huo kulikuwa na mlipuko wa homa kali ya mafua, inayoitwa Spanish flu' iliyosabisha vifo takribani 642, 000 ndani ya Marekani. Michezo iliendelea kwa tahadhari ya Ugonjwa huo kwa tamko la Rais wa Marekani wa wakati huo Woodrow Wilson kupitia barua ambayo iliwekwa hadharani 1919.Picha hii ilipigwa na mwanafunzi wa Georgia aliyeitwa Thomas Carter.
 
Ukifika HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI kuna wodi inaitwa Sewahaji. Unamjua Sewahaji alikuwa ni nani?"Sewa Haji Paroo ndio hasa alianzisha hospitali ya Muhimbili, Ingawa baadhi ya walioathiriwa na Elimu ya Kikoloni kwa kiwango kikubwa hushikilia kwamba Muhimbili ilianzishwa na Waingereza. Taarifa zilizopo Hospitalini Muhimbili na Makavazi ya Taifa ni kuwa SEWA HAJI PAROO toka India ndiye hasa Mwanzilishi wa Hospitali ya Muhimbili.Sewahaji alikuwa ni mfanyabiashara, na alikuja Afrika Mashariki kutafta Maisha. Alifika huku Tanzania Bara(Tanganyika) kupitia kisiwa cha Zanzibar akitokea katika mji wa Bhuj
 
Mwaka 1852 aliamua kufungua Duka la bidhaa mbalimbali kwenye Visiwa vya Zanzibar. Biashara ilikuwa kubwa zaidi, Hivyo mwaka 1860 alifungua Duka lingine kubwa maeneo yaBagamoyo, kisha akaamua kuweka Makazi yake hapo.Biashara zake ikawa kubwa mno, hivyo Sewahaji akawa ni mmoja kati ya matajiri wakubwa katika eneo la Afrika Mashariki.Alisaidia Watu wote bila kujali Rangi, Dini wala Kabila zao. Alinunua Majengo kadhaa na kuyafanya Makazi Watu wasiojiweza na wasio na makazi waliokimbilia Mzizima. Kwa wasiofahamu, Mzizima ndio Dar es salaam ya sasa. Hivyo basi ile hali ya watu kukimbilia Dar imekuwepo miaka na mikaka!
 
Alijenga shule za msingi na Hospitali kadhaa katika Mji Wa Mzizima (Sasa ni Jiji la Dar es Salaam)Alijenga Hospitali akaiita Sewahaji Hospitali ikawa inatoa Huduma bure kwa Walalahoi wa Mzizima.Mnamo Februari, 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo alifariki Dunia. Ilikuwa ni Huzuni na Simanzi kubwa wakazi wa Bagamoyo na Mzizima. Aliependwa sana kwa Moyo wake wa Ukarimu!Baada ya Kifo chake, Wakoloni wakabadilisha Jina Kutoka "Sewahaji Hospital" na ikaitwa "Princess Magreth Hospital".
 
Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo ya Wodi inaitwa SEWA HAJI. Kulingana na Kaka Manyerere Jackton, eneo ilipo Muhimbili ya sasa ilikuwa eneo la kutupia Masalia yanayotokana na Mama kujifungua. Na masalia hayo huitwa Muhimbili, hivyo hiki ndio chanzo cha Hospital hii kuitwa MUHIMBILI.

Leo jiulize mchango wako katika kuboresha hali ya watu wengine, Usijiulize kuhusu umaarufu kwani siku moja historia itasema yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…