IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa binadamu wa kawaida wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana ambao sisi tunawaita ni genius (watu wenye vipaji) wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea. U
Kutokana na mazingira tunayoishi IQ yako inaweza kupanda kutoka 90 kwenda 99 au kushuka toka 90 mpaka 70, kufanyia mazoezi ubongo wako inaweza kupelekea utanuke zaidi. IQ yako inaweza kuimarika zaidi kwa mfano kusoma vitu vya aina mbalimbali na pia kujifunza lugha tofauti.
Nimepima IQ za watu wengi nimeona ni hafifu sana kwa mfano unaweza kuta katika magroup/pages fulani za udaku imepostiwa picha ya mrembo kwa juu ikiwa na maneno Comment na share Mara 5 picha yangu ntakufata inbox nikupe namba wangu⦠kiukweli ni zaidi ya mamia ya watu wanafanya hivyo wakiamini ni kweli watapata wanachokitaka kutokana na picha husika. Mtu anapost kwamba hizi ni simu ambazo Dangote anagawa ukitaka kupata share mara 5 na like kisha utapata hii simu. Kama ushawahi kufanya hivyo basi IQ yako ina matatizo.
Terrence Tao ni mwanahisabati kutoka Marekani ambaye anakadiriwa kuwa na IQ level ya 230. Terence Tao aliweza kufanya hisabati akiwa na miaka 2 na alipokuwa na miaka 7 aliweza kufanya hesabu ngumu za level ya Chuo Kikuu akiwa na miaka 20 alipata PhD. Mwaka 2006 alishinda medali ya Field na mwaka 2014 alipata tuzo ya Breakthrough prize in mathematics .
Hivyo basi Linda IQ yako iweze kuimarika siku hadi siku na sio kushuka, kuna makampuni mengi ya kitapeli yanacheza na akili zetu wanajua tuna IQ ndogo katika kufikiri na watakuja kukwambia toa laki 5 kisha utafaidika kila siku unavyoingiza watu kwa upande wako wa kulia na kushoto yani kama matawi na porojo nyingi kibao lakini baadae hutoona faida.
Wale ndugu zangu wa kama wewe ni mzuri bila ya make up tupia picha yako tuone uzuri wako tukupe maksi au taja umri wako wa kuzaliwa kama mmefanana nendeni inbox na wale wa kama simu yako Original Fanya kitu hiki kikitokea simu yako ni Original na bila ya kuwasahau wale wazee wa kubisha vitu bila ya kuwa na uthibitisho wowote zaidi ya mhemko tu basi tambua wewe ni katika watu ambao IQ zao ni ndogo sana katika hii dunia.
βKama unataka kuwa bora basi jitambue wewe ni nani weweβ