Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Duh!!
 
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amethibitisha kuwa Seneta mmoja na msaidizi wa seneti nchini Madagascar wamefariki dunia leo kutokana na Ugonjwa wa Covid19.

Rajoelina ameongeza kuwa maseneta wengine 14 na wasaidizi 11 nchini humo wanaugua ugonjwa huo. Mpaka sasa watu 5,080 wameugua virusi vya Corona nchini humo, na watu 37 wamefariki dunia. Kuanzia jana hadi leo watu 213 wamekimbizwa hospitali wakiwa mahututi.

Wiki iliyopita serikali nchini humo iliweka tena zuio la kutoka nje (lockdown) kwa wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mji mkuu wa Antananarivo, kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.

#MyTake;
Vipi ile "sample" tuliyoambiwa inachunguzwa na majibu tutapewa ndani ya wiki mbili? Je wiki mbili hazijaisha au ilimwagwa kimyakimya? Na vp mafuta ya bombadier zetu zilizotumika kwenda kufuata togwa la Madagascar? Wataturudishia? Ma je wale waliosema ile togwa sio dawa wakaitwa mawakala wa mabeberu, je wataombwa radhi? Na vp wale waliokunywa ile dawa kwa tashwishwi, watapewa dawa ya kusafisha tumbo au ndo basi tena?
Malisa GJ
 
Mwaka 2011 madaktari walisema kuwa Fagilyu Mukhametzyanov, kutoka Kazan, Urusi, ameshafariki lakini kumbe alikuwa amezirai na alikuja kustuka wakati anakaribia kuzikwa. Alipatwa na mstuko wa moyo na akakimbizwa Hospitali lakini alikufa ndani ya dakika 12, Safari hii ikiwa ni kifo cha kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…