Anaitwa James Lewis Jackson raia wa Texas US ambaye February 2007 alinyongwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa alikuwa mhusika mkuu wa mauwaji ya mkewe pamoja na watoto wawili wa kike wa kufikia.
Mauwaaji hayo ambayo hata yeye mwenyewe alikiri kuyafanya alisema aliyafanya April 1997 kwa kumuuwa mkewe Sharonon (39) pamoja na mabinti zake wawili wa kufikia Ericka Mayes (18) na Sonceria Mayes (19).
Katika nyumba waliyokutwa ndugu hawa wamefariki kulikutwa karatasi iliyoandikwa na James mwenyewe iliyokuwa na maandiahi "Sikuweza kuijali na kuihudumia familia yangu, sikuwa na kazi, nimeamua kuwarudisha kwa Mungu, naamini Mungu atanielewa, nao watanielewa".
James alinyongwa mwaka 2007 alikwa na umri wa miaka 47.