Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Asali na maziwa ya unga

Chukua kikombe, weka maziwa ya unga kijiko kimoja, asali kijiko kimoja na juisi ya limau nusu kijiko. Changanya kisha paka usoni na usugue taratibu. Acha usoni kwa dakika 15 na kisha osha taratibu kwa maji fufutende.

Utayaona matokeo baada ya muda mfupi.
 
Mchanganyiko wa matunda

Chukua tango, nanasi na papai bichi; visage.

Mchangayiko laini utakaopatikana hapo ndiyo dawa yako.

Usugue uso wako taratibu kutoka chini yaani kidevu ni kwenda juu.

Uache ukae usoni kwa dakika 20 kisha osha kwa maji ya baridi.
 
Screenshot_20200728-110651.png

Playmaker + Golden glove
 
  1. wewe muhuni ile project ya wafaransa nitaipatia wapi?
  2. messiah haijanivutia ila imemaliza vizuri baada ya tukio la kuanguka kwa ndege(ameonyesha muujiza kwa wasiomuamini)
  3. Raymond "Red" Reddington akianzisha dini nitakuwa mfuasi wake, hatimaye season 1 nimeimaliza...... najipanga kuitafuta season 2 ya the blacklist
  4. usisite kuniongezea pombe nyengine
 
Sugar Ray [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Mzee wa pwani umenikumbusha mbali sana... Ilikuwa kama kichocheo yaani, baada ya mida mida ni kuvuka barabara kichochoro cha kwanza tu Wahay...hawa hapa wamejipanga. Unatia timu kwa bonge mweusi [emoji1][emoji1][emoji1]

Eti hawa hapa wamejipanga [emoji16][emoji16][emoji16]

Umenikumbusha kisa fulani hivi. Basi siku moja bro huyoo akanikokota. Mi bado mdogo sijayajua hayo mambo vizuri. Kulikuwa na mtaa mmoja mashuhuri sana pale mjini kwetu unaitwa mtaa wa Mzee Fundikira. Haoo mpaka nyumba mojawapo kuu kuu imechoka choka hivi. Chumba cha tatu kulikuwa na binti mdogo mzuri sana amekaa nje ya mlango wa chumba amejifunga kanga. Bro akaniambia we nenda kwa huyo mi naingia hapa kuna mpya kaja juzi tu. Akazama na kuniacha kwenye veranda nang'aa macho. Binti yule akanikaribisha. Kuingia ndani binti akaiweka kanga kwenye kamba. Uwiii alikuwa bado mbichi kabisa yaani kifuani saa sita halafu cheusi umbo mkatiko. Wakati nashangaa shangaa, mlolongo wa maswali ukaanza:

"Una shilingi ngapi? Unataka kufanya nini? Bei unazijua?"

Nikawa nang'aa macho tu kwa sababu bro hakunipa cho chote. Binti akajifunga kanga yake tukatoka nje. Akaniambia nikamsubiri niliyekuja naye kando ya barabara huko.

Baada ya muda bro akaibuka jasho linamtoka. Kumuuliza mbona umeniacha bila pesa akasema alisahau. Kuanzia siku hiyo ndo nikaujua mtaa wa Mzee Fundikira na yaliyokuwa yakifanyika huko.

Ila last born miye nilichokosea ni kumpa hii stori dadangu mmoja aliyekuwa rafiki yangu sana. Kumbe naye akaenda akamwambia mama. Aisee nilipigwa mkwara mkali sana japo wakati ule hata UKIMWI haukuwepo. Halafu baadaye nikagundua kuwa bro alikuwa anajua dawa fulani hivi ya mitishamba ya kutibu gono. Alikuwa anaitengeneza anapiga kwenye lichungu likubwa hapo nje tu. Siku nzima lipo hapo linatokota. Halafu kesho yake utamuona na baadhi ya marafiki zake wanajichotea na kunywa kwa kadri wawezavyo. Kumbe ndiyo wanajitibu...

Dunia ya wakati ule ilikuwa tofauti sana na watani zangu hao nilikuja kuwaelewa vizuri baada ya kwenda huko kusoma fomu siksi. Ila wakati ule Juliana aka UKIMWI ndiyo ulikuwa unaingia na hali haikuwa shwari kivile. Na waliojifanya vijogoo aisee hawakusalimika. We lost a lot of boys [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom