Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuanzia Mwakani 2021 shirika la anga la Marekani NASA litaanzisha utalii wa nje ya dunia ambapo utaweza kulipia $125,000 na kisha kuanza safari ya masaa 6 hadi nje ya dunia kutalii kwa kutumia usafiri, baloon maalumu. utakaa hadi wiki mbili huko. hii ni zaidi ya milioni 290 za Tanzania. Utalii huu umekuwa ukifanywa tangu miaka iliyopita kwa watu binafasi kulipa mamilioni ya pesa kwenda kutalii huko, lakini haikua rasmi. Tazama Video. Sasa NASA wamepanga kuanzia mwakani 2021 Space Tourism iwe rasmi kabisa kwa gharama ya wastani inayotajwa kuwa kati ya $125,000 hadi $250,000 kwa mtu mmoja kutegemea na muda mtakaokaa huko.
 
Adam (39) na Anne (37) wote ni waigizaji wakubwa tuu wa filamu US, kama unazifahamu filamu za Married Life (2007) au The Chaperone (2018) basi ni baadhi ya filamu alizoshiriki kuigiza Adam, ni mtayarishaji wa filamu pia. Anne yeye kafanya movies nyingi sana kama The Devil Wears Prada (2006) na The Intern (2015). Adam amefanana sana na aliyewahi kuwa mwandishi wa mashairi, mtunzi na mwigizaji William Shakespeare raia wa Uingereza aliyezaliwa mwaka 1564 na kufariki mwaka 1616. Umaarufu zaidi wa William miaka hiyo ulikuja baada ya kutunga shairi pendwa la "Bard of Avon" lililofikia hatua ya kupewa jina la shairi la taifa. Licha ya Adam kufanana sana na William (pichani) lakini pia hata William naye mkewe aliikuwa anaitwa Anne Hathaway kama ilivyo kwa Adam.
 
Wanasayansi hao walikuwa ni mwanamama Luella pamoja na Winthrop Kellogg wote raia wa Indiana US. Sokwe huyo alikuwa anaitwa Gua, alizaliwa November 15, 1930 huko Havana, Cuba na kulelewa na mama yake Pati na baba yake Jack. Baada ya mama yake Pati kufariki Mei 13, 1931 Gua akachukuliwa na mtaalamu wa waanyama Madam Rosalia Abreu na kumpeleka katika hifadhi ya Orange Park, Florida US. Baada ya kufikisha mwaka 1 ndipo Gua akachukuliwa na wanasaikolojia Luella pamoja na Winthrop Kellogg waliompeleka nyumbani kwaajili ya tafiti mbalimbali kumhusu sokwe huyo, mara zote walikua wanamtunza nyumbani kwa Kellogg. Gua aliyekuwa sokwe wa kike alianza kuzoeshwa kuishi na mtoto wa kiume wa Kellogg wa umri wa miezi 10 aliyekuwa anaitwa Donald huku akiwakuza kwa pamoja na kama dada na kaka akiwapa huduma sawa. Lengo lake ilikuwa ni kuona kama sokwe anaweza kujifunza na kuishi kwa tabia za kibinadamu? Kwasababu Donald na Gua wote walikuwa na umri sawa, hivyo mafunzo aliyokuwa akiwapa wote kwa pamoja alitegemea yangeshikwa kwa wote. Baada ya miezi 9 kupita matokeo yalikuwa tofauti, Gua alikuwa anaweza kumtambua mtu kwa harufu yake na rangi ya nguo wakati Donald alikuwa anaweza kumtambua mtu kwa sura yake, Donald alikuwa ameanza kuongea huku Gua akiwa haongei. March 28, 1932 Kallogg akaamua kufutilia mbali utafiti huo baada ya kuona sasa mambo yamekua tofauti, badala ya Gua kuiga tabia za binadamu, mwanaye Donald ndiye aliyeanza kuiga tabia za Gua. Gua akarudishwa katika hifadhi ya Orange Park alikofikwa na umauti December 21, 1933 baada ya kuugua Pneumonia wakati huo Donald alikuwa kafikisha miaka mitatu tayari.
 
Da'Vinci

Padre Pio ni mmoja wa viongozi wa dini maarufu sana kuwahi kutokea duniani anayetajwa kuwa alikuwa na imani kali sana ya dini yake, alikuwa muumini wa kanisa katoliki raia wa Italia, alizaliwa Mei 25, 1887 na kufariki September 23, 1968. Dalili za kuijua dini ndani yake zilianza kuonekana tangu akiwa mdogo kwani mara kadhaa alikuwa anadai kuwa amezungumza na malaika, Yesu pamoja na Bikra Maria. September 21, 1910 akiwa na umri wa miaka 23 wakati ametawazwa kuwa mtawa alitokewa na vidonda katika mikono na miguu yake mfano wa vidonda alivyovipata Yesu kutokana na kusurubishwa msalabani, vidonda hivyo alikaa navyo kwa miaka 58 bila kupona. Ajabu ni kwamba siku tatu tuu kabla ya kifo chake vidonda vyote vilipona. Padre Pio anaelezwa kuwa alikuwa ana uwezo wa kuisoma nafsi ya mtu na kujua mtu huyo anawaza vitu gani, na hata ilikuwa muumini ukienda kuungama dhambi kwake, baada ya kutaja madhambi yako anakwambia kabisa kuwa dhambi fulani na fulani umezisahau, tubu zote. March 21, 1912 Pio alimuandikia barua padre mwenzake Agostino akiandika mambo mengi ya kimiujiza ambayo Padre Agostino alikiri kutoelewa na ikaelezwa kuwa ni mambo yanayopatikana katika kitabu cha siri cha Maria Gemma aliyefariki mwaka 1903 akiwa na umri wa miaka 25. Kama ilivyo kwa Padre Pio, ndivyo alivyokuwa pia Maria, naye aliyapata makovu hayo June 8, 1899 akiwa na umri wa miaka 21, alidai pia kuwa huongea na malaika mbalimbali, Yesu na hata Bikra Maria ambao walikuwa wanampa jumbe kadhaa kuhusu mambo yajayo. Baada ya barua hiyo Padre Pio alikataa kwamba hana kitabu hicho kilichowahi kuandikwa na Maria ambaye aliitwa pia bikira Maria. September 20, 1918 Pio alikiri wazi kuwa katika maombi yake hakuwahi kuomba apone madonda hayo yakiwemo ya miguuni na mikononi kama mtu aliyepigiliwa misumali, licha ya kuwa yalikuwa na maumivu makali na kutoa damu kila siku lakini alisema anapenda anavyoteseka. Alisema kuwa damu zilizokuwa zikitoka katika madonda hayo alikuwa anazisafisha na manukato maalumu au maua, hali hii ya kupata vidonda kama hivi inaitwa Stigmata, inahusiana na imani za dini hasa Ukristo.
 
Pio Alimwambia Agostino kuwa anapata uchungu wa taji la miba na mara nyingi anapigwa mijeredi kimiujiza. Hakufafanua zaidi lakini alisema kuwa amekuwa akisumbuliwa nayo angalau mara moja kwa wiki. Kama ilivyo kawaida, wanasayansi ni lazima watie miguu katika kila jambo linaloonekana kuiteka dunia, walifanya uchunguzi wao katika hili pia na mwaka 1954 walisema kuwa madonda hayo Pio aliyatengeneza tuu mwenyewe kwa kujidondoshea asidi aina ya carbolic. Mwaka 1947 Padre Pio alimponya upofu msichana Gemma de Giorgi wa miaka 7 aliyesafiri na bibi yake hadi San Giovanni Rotondo kumuona Pio. Gemma alizaliwa bila pupils za macho hivyo kuambiwa hataweza kuona katika maisha yake yote. Mwaka 1947 pia Padre Pio alikutana na Padre Wojtyła wa Poland, mbali na mazungumzo mengine pia akamwambia ajiandae kuwa kiongozi mkubwa wa kanisa duniani, kweli mwaka 1978 Wojtyła akatangazwa kuwa ndiye Papa mpya wa kanisa katoliki duniani miaka 31 baada ya utabiri. Wojtyła ndiye Papa John Paul II aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 2005. Mwaka 1962 tena Padre Wojtyła alimuandikia barua Padre Pio akimuomba kumuombea rafiki yake Wanda Półtawska aliyekuwa anaugua kansa huku akiambiwa kuwa amebakiza miezi 18 tuu ya kuishi, baada ya Pio kupokea barua hiyo alimuombea, na kansa ikapotea. Wanda aliyezaliwa mwaka 1921 yuko hai mpaka sasa, ni mwandishi na mwanafizikia kutoka Poland, aina hii ya kansa kupotea kimaajabu inaitwa Spontaneous Remission, hata madaktari walishindwa kuelezea imekuwaje Wanda hana kansa tena. September 21, 1968 akiwa anatimiza miaka 58 tangu apatwe na Stigmata, Pio hali yake ilianza kuwa mbaya, hatimaye akafariki siku mbili baadaye September 23, 1968 akiwa na umri wa miaka 81. Ajabu ni kuwa ndani ya siku hizo tatu hali yake ianze kuwa mbaya vidonda vyake vilipona kabisa. March 3, 2008 ikiwa ni miaka 40 imepita tangu afariki kaburi lake lilianza kuumuka hali iliyopelekea mabaki ya mwili wake kuondolewa kaburini humo na sasa yapo katika sehemu maalumu ya makumbusho mjini San Giovanni Rotondo in Italy.
 
Jodie aliyezaliwa mwaka 1990 alianza kuonekana na tatizo hilo mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka mitatu na hatimaye mwaka huo 1993 akiwa na miaka hiyo 3 akafanyiwa upasuaji wa kuondolewa nusu ya ubongo. Inaelezwa kuwa upande mmoja wa mwili wake haukuwa unafanya kazi, ulipooza na hata akikaa basi mwili utaelemea upande mmoja mfano wa mzani unavyoelemea upande mmoja unavopima kitu. Hali hiyo ilipelekea madaktari kusema kuwa njia pekee ni kumfanyia upasuaji na kuondoa nusu ya ubongo, ni kweli aliondolewa na hadi sasa yuko sawa kabisa. Tatizo hili huwapata zaidi watoto wa chini ya miaka sita. Wataalamu wanasema kuwa inawezekana kuishi na ubongo nusu au hata chini ya nusu.
 
Ukifika mjini Yates, New York US moja ya story za kustaajabisha utakazokutana nazo ni pamoja na story ya kuhusu sura ya mwanamke Matilda Gillette iliyokuwa ikijichora kwa rangi nyeupe katika kaburi lake mwenyewe miezi kadhaa baada ya kuzikwa mwaka 1936. Matilda alizaliwa mjini hapo mwaka 1859, baadaye akaolewa kwa mwanaume Francis aliyekuwa amemzidi miaka 9. Maisha yaliendelea na kila kitu kilikuwa sawia kabisa. Mwaka 1936 Matilda alifariki na kuzikwa katika makaburi ya Lakeview Cemetery barabara ya West Lake huko Yates, lakini miezi kadhaa baadaye jambo la ajabu lilitokea kwani sura ya Matilda ilijichora kwenye jiwe ubavuni mwa kaburi lake. Wanasema kuwa mji haukosi wazee, kutokana na wazee wenyeji wa mji huu hapa kukapatikana stori tofauti tofauti juu ya kwanini sura ya marehemu ilijichora yenyewe katika kaburi lake
 
Story ya I: Francis na Matilda walipendana sana kiasi cha kufikia hatua ya kuahidiana kuwa mmoja akifariki basi atakaebaki hatakua na mwenza mwingine kitendo ambacho Francis alikaidi, kwani baada ya Matilda kufariki alipata mwanamke mwingine. Miezi kadhaa tuu baada ya Francis kuoa katika kaburi la Matilda kulianza kuonekana sura yake inajitokeza ubavuni mwa jiwe ikiwa kama imelala hivi, jamaa akaamua kuvunja kaburi na kulijenga upya, lakini bado sura ikajitokeza tena.
 
Story ya II: Wakati wakiishi pamoja Francis hakuwa mume mzuri, alikuwa mkatili na mwenye tabia za ajabu, kutokea kwa sura ya Matilda kaburini kwake ilikuwa ni kuonyesha masikitiko yake kwa mumewe huyo kila alipokuwa akitembelea. Story ya III: Matilda alitumia muda mrefu sana kuugua kitandani kabla ya kifo jambo lililokuwa likimkera sana Francis, hakua anamjali Matilda, alifariki akiwa na huzuni juu ya upendo mdogo wa mumewe, hii ndio sababu ya sura yake kujichora katika kaburi lake. Licha ya sababu hizi zote kutajwa lakini hakuna uhakika ulioripotiwa kuwa ndio sababu halisi kwa asilimia zote, lakini baada ya Francis pia kufariki sura hiyo ikapotea, kaburi lipo hadi sasa.
 
Taarifa ya mtandao wa Mirror Iliyochapishwa July 21, 2020 ilisema kuwa mwanamke Heni Nuraeni raia wa Tasikmalaya, Java Indonesia alipatwa na sintofahamu baada ya kujifungua mtoto ikiwa ni ndani ya lisaa limoja tuu tangu ajihisi ni ujauzito. Heni mwenye umri wa miaka 28 na mama wa watoto wengine wawili alisema kuwa bado haelewi ni nini kilitokea hadi ikatokea hali hiyo ya ndani ya lisaa limoja tuu ajihisi mjauzito, apate uchungu na ajifungue mtoto wa kiume. "Mwanzoni nilipokuwa nyumbani hakukuwa na kitu chochote cha kushangaza, ghafla nikahisi kitu kinatembea upande wa kulia wa tumbo langu, na nikapelekwa nyumbani kwa baba yangu, ndani ya lisaa limoja nikajifungua" Heni anasema kuwa mwanzo hajawahi jihisi kuwa ni mjamzito kwasababu hakukuwa na dalili yoyote aliyoipaya, na hata mzunguko wa hedhi alikuwa akiupata kila mwezi kama kawaida. Dkt. Ruswana Anwar wa hospitali ya Bandung’s Hasan Sadikin alisema kuwa kuna vitu havikuwa sawa katika mwili wa Heni na tatizo kama hilo hutokea kwa nadra sana, aina hii ya ujauzito inaitwa Cryptic Pregnancy. Dokta alisema kuwa mwanamke kuendelea kupata hedhi wakati ni mjamzito ni ukosefu wa usawa wa homoni, lakini alisisitiza kwamba haiwezekani kwa mwanamke kujifungua baada ya saa moja tu ya kujitambua kuwa mjamzito.
 
Inaitwa Venetian Ceruse au Blanc de ceruse de Venise, haya yalikuwa ni mafuta ya urembo, makeup maarufu sana iliyokuwa ikitumiwa na wanawake wa familia za kitajiri katika karne ya 16, makeup hii ndiyo iliyopelekea kifo cha malkia Elizabeth I wa Uingereza. Elizabeth I ni malkia aliyeitawala Uingereza kwa miaka 44 kati ya mwaka 1558 hadi anafariki March 24, 1603 akiwa na miaka 69. Miaka 31 baada ya kifo chake ilibainika kuwa makeup hiyo iliyokuwa kama poda nyeupe aliyokuwa anapenda sana kuipaka usoni ndiyo iliyomuuwa kwani sumu yake ilikuwa ikipita kwenye ngozi mpaka kwenye damu. Historia imeandika kwamba Elizabeth alikuwa ni mtoto wa mwisho katika familia, hakuwahi kuwa na mtoto na hadi anafariki akiwa na umri huo wa miaka 69 alikuwa bado bikra, hakuwahi kuolewa wala hakuwahi kukutana na mwanaume. "Na mwisho, hii itakuwa ya kukumbukwa kwangu, kwamba jiwe, mwanamke shupavu alitangazwa kuwa malkia, baada ya kutawala wakati wote, aliishi na akafa bikira" Kauli hii aliitoa mwaka 1559 akiwa na mwaka mmoja tuu madarakani. Begi lake la kwapani, handbag lilikuwa linamsaidia kutoa taarifa kwa walinzi wake, mfano kama anataka kuondoka, kumaliza mkutano dakika tano zijazo, basi ataweka begi lake mezani, na popote atakapokwenda lazima huwa nalo. Lakini kwa ishara nyingine pia alikuwa anaweza kubadilisha mkono wa kushika handbag yake hiyo nk, inaelezwa kuwa njia hii ya mawasiliano kwa kutumia handbag pia inatumika na malkia Elizabeth II anayeiongoza sasa Uingereza. Mbali na makeup hii kumuuwa Elizabeth I lakini pia inatajwa kuwauwa wanawake wengine wengi maarufu kama Maria Gunning.
 
Gulileo likuwa mwana anga na injinia maarufu kutoka Italia, alizaliwa February 15, 1564 na kufariki January 8, 1642 Arcetri, Italia akiwa na miaka 77. Huyu ndiye mgunduzi wa miezi ya sayari ya Jupiter, sayari hii inatajwa kuwa na miezi 79. Katika miezi hiyo 79 iliyothibitishwa na shirika la anga la Marekani NASA, Gulileo aligundua miezi minne iliyopewa jina la miezi ya Gulileo yaani Gulileo Moons ambayo ni Io, Ganymede, Europa na Callisto. Mbali na hilo pia Gulileo anatajwa kuwa ndiye mgunduzi wa saa ya mshale. Miaka 95 baada ya kufariki jino lake moja na vidole vyake vitatu kikiwemo kidole cha katikati cha mkono wa kulia viliondolewa na kuhifadhiwa katika makumbusho ya kihistoria ya Museo Galileo, Italia. Sababu ya kuondolewa ni kumbukumbu na upendo tuu. Taarifa ya mtandao wa The Guardian ya Juni 8, 2010 ilisema kuwa muongozaji mkuu wa makumbusho hayo alitangaza kuwa maonyesho hayo yanaonyesha vidole viwili, kidole gumba na kidole cha kati vya Gulileo. Mbali na vidole hivyo pia alisema wameanza kuonyesha jino lake moja ambavyo vyote vipo ndani ya chupa ndogo za vioo huku akisema kuwa kuna kidole chake cha tatu pia ambacho hicho hawatakionyesha. Mwaka 1737 kundi la watu waliokuwa wanampenda Gulileo waliuvamia mwili wake mahala ulipokuwa umehifadhiwa na kuondoka na vidole vitatu pamoja na jino moja na kwenda kuvihifadhi katika chuo kikuu cha Padua alikokuwa anafundisha enzi za uhai wake. Hata hivyo baada ya viungo hivyo kukaa kwa miaka mingi, mwaka 1905 viliripotiwa kuwa vimeibiwa chuoni hapo. November 23, 2009 Mtandao wa CNN ulitoa taarifa kuwa vidole hivyo pamoja na jino moja vilivyokuwa vinasimamiwa na Paolo Galluzzi chuoni hapo vilivyoibiwa tangu mwaka huo wa 1905 vilikuwa vimepatikana tena. Taarifa zaidi zilisema kuwa Paulo mwenyewe aliamua kuviuza ili ajipatie pesa, na hatimaye sasa vilikuwa vimepatikana baada ya ufuatiliaji mkubwa wa hati za mauziano, vilianza kuonyeshwa hadharani katika makumbusho hayo. Moja kati ya quotes zake aliwahi kusema kuwa "sijawahi kukutana na mtu yeyote na nikashindwa kujifunza lolote kutoka kwake"
 
Anaitwa Desmond Thomas Doss aliyezaliwa Virginia US February 7, 1919 na kufariki March 23, 2006 akiwa na miaka 87. Huyu alikuwa mmoja wa wanajeshi wa US aliyeingia vitani na wenzake katika vita ya Okinawa Japan mwaka 1945 ambayo ilikuwa ni sehemu ya vita ya pili ya dunia. Desmond aliingia vitani bila silaha kwasababu yeye alipewa kitengo cha utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanajeshi wenzake waliokuwa majeruhi, lakini mwisho wa vita alionekana ni shujaa aliyewaokoa wenzake 75 katika uwanja wa vita. Ukitazama movie ya kivita ya Hacksaw Ridge iliyotoka mwaka 2016 imechezwa kufuatisha story nzima ya Desmond, na shujaa kwenye movie hiyo ni Andrew Garfield aliyecheza kama Desmond. Kutokana na ushujaa huo Desmond anatajwa kuwa ni mmoja wa wanajeshi wa kuheshimika zaidi katika jeshi la Marekani, kabla hajafariki mwaka 2006 alikuwa amepokea tuzo nyingi za heshima. J
 
Tunafahamu kwamba Uingereza inaongozwa kifalme na kimalkia, na malkia wa sasa wa Uingereza ni Elizabeth II aliyeingia madarakani mwaka 1952, kabla yake alikwepo mfalme George VI ambaye alivyofariki tuu ndipo akaingia Elizabeth. Kabla ya George VI kulikuwepo na mfalme Edward VIII aliyetawala kwa muda wa miezi 12 tuu kati ya January 1936 na December 1936, huyu aliacha ufalme mwenyewe na kuandika historia ya kuwa mtawala wa kwanza wa Uingereza kuachia ufalme kwa hiari yake mwenyewe. Kwanini Aliacha? Kisa ni mapenzi. Ilikuwaje? Edward alikuwa mtoto wa mwisho katika familia, baba yake George V ndiye alikuwa mfalme wa Uingereza, na alikuwa anampenda sana mwanaye huyu hadi kufikia kusema wazi kuwa akifariki yeye basi mwanae huyu wa mwisho ndiye arithi ufalme. Ni kweli baada ya baba yake kufariki January 20, 1936 Edward VIII akaingia madarakani kama mfalme mpya, lakini wakati anaingia alikuwa ameanza kupendana na mwanamke wa kimarekani Wallis Simpson ambaye walikuwa wanajuana tangu miaka mitano nyuma. Edward alitaka kumuoa Wallis, lakini shida ikaja kwa familia na viongozi wengine wa nchi wakisema kuwa Uingereza haiwezi kuwa na malkia kutoka Amerika, kwahivyo Edward hawezi kumuoa mrembo huyo wa kimarekani. Ilifika kipindi Edward alishutumiwa kuwa anataka kumuoa mwanamke wa kimarekani na kumfanya malkia ili kuiangamiza Uingereza, walihofia anaweza kuwa mpelelezi aliyetumwa kuichunguza Uingereza, hii ilipelekea kujihuzuru kwa viongozi wengi wa serikali. Edward aliona isiwe tabu, baada ya kukaa miezi 12 madarakani December 11, 1936 akaamua kutangaza rasmi kuwa anaachia kiti cha ufalme ili awe huru kumuoa mwanamke anaempenda huku akisema kuwa hawezi kuwa mfalme bila yeye, ni kweli aliacha, na Juni 7, 1937 wakaoana. Kaka yake George VI ndiye alichukua kiti cha ufalme ambapo naye baada ya kuariki mwaka 1952 akamuachia ndugu yake Elizabeth II ambaye ndiye malkia hadi sasa. Edward alifariki mwaka 1972 na Wallis alifariki mwaka 1986.
 
Jengo Hili Lililojengwa Mwaka 1732 Lipo ndani ya Eneo Kubwa tuu la Kihistoria Huko Pune Katika Mji wa 'Maharashtra' Magharibi mwa INDIA, Eneo hilo Lote Limefungwa Kutembelewa Usiku Kwa Miaka Kadhaa Sasa na Sababu ni Hiyo ya Mambo ya Kutisha. Mbali na Jengo hili Kuhusushwa na Mambo ya Mapigano Kakini pia Lilikuwa Likitumika Kufanyia Shughuli Mbalimbali za Kijadi Hapo Kale. Inaelezwa Mashujaa na Viongozi Wengi wa Kuvita Hapo Kale Walizikwa Humo na Mizimu yao Bado Ipo Mpaka sasa na Husikika Zaidi Nyakati za Usiku. Inasemekana Kwama Hua Zinasikika Sauti nyingi za Ajabu ajabu Nyakati za Usiku na Moja ya Sauti hizo Husikika Ikisema "KAKA MALA VACHWA" Yenye Maana ya "Uncle Save Me" na Wengi Waliozisikia Sauti hizo Wamekuwa Wakiugua UKICHAA. Historia Imeandika Kwamba Mmoja wa Majenerali na Mashujaa wa INDIA wa Hapo Kale "Baji Rao I" Alikuwa na Ndoto za Kujenga Ngome Kama hiyo Itakayomsaidia Kuandaa Jeshi Lake na Kujilinda Katika Mapigano, Alianza Kujenga 1730 na Kumaliza 1732. Wakati wa Mapigano Aliuliwa na Baadae Watoto Wake Watatu pia Kuuliwa Ndani ya Ngome hiyo, Mtoto wa Mwisho Kuuliwa Alikuwa na Umri wa Miaka 16 na Inaelezwa kuwa Wakati Ameshikiliwa Alikuwa Akipiga Kelele Kuomba Msaada "Uncle Save Me". . Moja ya mastaa waliohusika kwenye movie hiyo ni mrembo Priyanka Chopra
 
Anaitwa James Lewis Jackson raia wa Texas US ambaye February 2007 alinyongwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa alikuwa mhusika mkuu wa mauwaji ya mkewe pamoja na watoto wawili wa kike wa kufikia. Mauwaaji hayo ambayo hata yeye mwenyewe alikiri kuyafanya alisema aliyafanya April 1997 kwa kumuuwa mkewe Sharonon (39) pamoja na mabinti zake wawili wa kufikia Ericka Mayes (18) na Sonceria Mayes (19). Katika nyumba waliyokutwa ndugu hawa wamefariki kulikutwa karatasi iliyoandikwa na James mwenyewe iliyokuwa na maandiahi "Sikuweza kuijali na kuihudumia familia yangu, sikuwa na kazi, nimeamua kuwarudisha kwa Mungu, naamini Mungu atanielewa, nao watanielewa". James alinyongwa mwaka 2007 alikwa na umri wa miaka 47
 
January 26, 1972 mwanamke wa umri wa miaka 22 Vesna Vulovic raia wa Serbia alinusurika katika ajali mbaya ya ndege ya JAT Yugoslav Flight 367 iliyolipuka angani ikiwa umbali wa futi 33,000 kutoka ardhini. futi 33,000 ni zaidi ya kilomita 10, ilikuwa na abiria 23 na wafanyakazi 5. Siku hiyo ya safari Vesna hakutakiwa kuwepo katika ndege hiyo, alipanda kutokana na makosa ya kuchanganya tiketi, kulikuwa na abiria mwingine aliyekua anaitwa Vesna Nicolic, huyu ndiye alitakiwa kuwemo katika ndege hiyo. Ndege hiyo ilikuwa inatoka Serbia kwenda Denmark, inaelezwa kuwa kundi la magaidi waliweka bomu kwa siri ndani ya ndege hiyo na ndiyo lililopelekea mlipuko huo saa chache baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Belgrade Serbia. Ndege iliripuka angani na kukatika katikati, kipande cha mbela kilianguka chini huku kipande cha nyuma kikianguka pia baada ya dakika tatu, tazama video katika post iliyopita, Picha zaidi zipo Telegram. Vesna alionwa na mwanaume mmoja raia wa Ujerumani aliyekuwa mtu wa kwanza kufika katika eneo la ajali, alimpa huduma ya kwanza hadi pale msaada kamili ulipofika. Baada ya uchunguzi madaktari walipoteza kabisa matumaini ya kwamba Vesna anaweza kupona, alikuwa amevunjika miguu yote miwili, alivunjika uti wa mgongo na pamoja na fuvu, Alikuwa amezimia pia. Baada ya siku tatu hospitalini Vesna alizinduka, kitu cha kwanza kuzungumza alisema anaomba sigara, alikuwa amepooza nusu ya mwili wake kuanzia kiunoni hadi chini. Hakuwa anakumbuka chochote kilichotokea mpaka alipokuja kuambiwa baada ya wiki mbili. "Wengi wanasema kuwa nina bahati, wanakosea, sina bahati, kama ningekuwa nina bahati basi nisingekuwepo katika ajali" Baada ya matibabu ya miezi kadhaa Vesna Alipona kabisa na kuendelea na maisha yake. Alikuja kufariki December 23, 2016 mjini Belgrade Serbia akiwa na umri wa miaka 66.
 
January 26, 1972 mwanamke wa umri wa miaka 22 Vesna Vulovic raia wa Serbia alinusurika katika ajali mbaya ya ndege ya JAT Yugoslav Flight 367 iliyolipuka angani ikiwa umbali wa futi 33,000 kutoka ardhini. futi 33,000 ni zaidi ya kilomita 10, ilikuwa na abiria 23 na wafanyakazi 5. Siku hiyo ya safari Vesna hakutakiwa kuwepo katika ndege hiyo, alipanda kutokana na makosa ya kuchanganya tiketi, kulikuwa na abiria mwingine aliyekua anaitwa Vesna Nicolic, huyu ndiye alitakiwa kuwemo katika ndege hiyo. Ndege hiyo ilikuwa inatoka Serbia kwenda Denmark, inaelezwa kuwa kundi la magaidi waliweka bomu kwa siri ndani ya ndege hiyo na ndiyo lililopelekea mlipuko huo saa chache baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Belgrade Serbia. Ndege iliripuka angani na kukatika katikati, kipande cha mbela kilianguka chini huku kipande cha nyuma kikianguka pia baada ya dakika tatu, tazama video katika post iliyopita, Picha zaidi zipo Telegram. Vesna alionwa na mwanaume mmoja raia wa Ujerumani aliyekuwa mtu wa kwanza kufika katika eneo la ajali, alimpa huduma ya kwanza hadi pale msaada kamili ulipofika. Baada ya uchunguzi madaktari walipoteza kabisa matumaini ya kwamba Vesna anaweza kupona, alikuwa amevunjika miguu yote miwili, alivunjika uti wa mgongo na pamoja na fuvu, Alikuwa amezimia pia. Baada ya siku tatu hospitalini Vesna alizinduka, kitu cha kwanza kuzungumza alisema anaomba sigara, alikuwa amepooza nusu ya mwili wake kuanzia kiunoni hadi chini. Hakuwa anakumbuka chochote kilichotokea mpaka alipokuja kuambiwa baada ya wiki mbili. "Wengi wanasema kuwa nina bahati, wanakosea, sina bahati, kama ningekuwa nina bahati basi nisingekuwepo katika ajali" Baada ya matibabu ya miezi kadhaa Vesna Alipona kabisa na kuendelea na maisha yake. Alikuja kufariki December 23, 2016 mjini Belgrade Serbia akiwa na umri wa miaka 66.
 
Anaitwa 'Margorie McCall' au Kwa Jina Maarufu la 'Lady with the Ring' Aliyeishi Katika Karne ya 18 Katika Mji wa Lurgan Kaskazini mwa Ireland, Inaelezwa Alifariki Mwaka 1705 na Akazikwa na Vitu Vyake vya Thamani Ikiwemo Pete yake Aliyoivaa. Muda Mfupi baada ya Kuzikwa, Kuna Mwizi Alitokea na Kuanza Kufukua Kaburi hilo kwa Kutaka Aibe Pete hiyo ya Bei mbaya, Baada ya Kuufukua Mwili Akajaribu Kuichomoa Pete Kidoleni lakini Alishindwa Kuitoa!, Ilikuwa Ngumu Kutoka. Maamuzi Yaliyomjia Baada ya Hapo ni Kukata Kabisa Kidole Ili Akaitoe Pete, Ndipo Alipostaajabu Kuona Marehemu Anaamka!, Inaelezwa Kuwa Jamaa Alikimbia Hadi Alienda Kufa kwa Mshtuko Mbeleni!. Historia Imeandikwa Kuwa Margorie Alizikwa Kimakosa, Alizikwa Akiwa Bado Mzima Baada ya Kuumwa Homa na Kuaminika kuwa Amefariki, Akainuka na Kurudi Nyumbani Usiku huo, Alipofika Ndugu zake Akiwemo Mumewe 'John McCall' Wakaanza Kukimbiana Wakihisi Labda Ulikuwa Mzimu wake. Baada tuu ya Kufika Nyumbani Aligonga Mlango na Kabla ya Kufungua Mlango Mumewe Alisikika Akiwambia Wanawe 'Kama Mama yenu Angekuwa Hai Basi Nauhakika Huyo Ndiye Angekua Anaegonga', Jamaa Baada ya Kuinuka na Kufungua Mlango Akakuta Kweli ni Mkewe!, Akapata Mshtuko Akafa. Inaelezwa Kuwa Baada ya Mumewe Kufariki kwa Mshtuko Baadae Familia Ilijiridhisha Kwamba ni Kweli Haukuwa Mzimu Bali Alizikwa Akiwa Hai. Maisha Yakaendelea na Akafanikiwa Kupata Watoto Wengine Miaka ya Baadae na Mwanaume Mwingine. Kaburi Lake Linapatikana Katika Eneo la Makaburi la 'Shankill Graveyard' lililopo Katika Mji huu wa Lurgan Kaskazini mwa Ireland, Limeandikwa 'Lived Once, Buried Twice' Yakiwa na Maana ya Aliishi Mara Moja, Alizikwa Mara Mbili!.
 
Back
Top Bottom