Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

December 21, 2018 mtandao wa The Sun wa Uingereza uliripoti taarifa ya mwanaume Khurum Shazada wa umri wa miaka 23 raia wa Birmingham nchini humo aliyekamatwa akifanya mapenzi na maiti saa chache baada ya kuzikwa. Hili ni tatizo la kiafya linaloitwa Necrophilia ambapo mtu anakua anatamani kushiriki tendo la ndoa na watu waliokufa ambapo hadi Shazada anashikiriwa alikuwa ameshafanya mapenzi na zaidi ya maiti 100. "Ninalala juu yao na kisha kuvuta suruali yangu," aliiambua mahakama. Mkewe alikiri kuwa ni kwa miezi mingi mumewe huyo alikuwa akirudi usiku nyumbani huku akinuka pombe pamoja na mnuko wa mtu aliyetoka kufanya mapenzi. Tabia yake hiyo alisema alianza kuwa nayo tangu mwaka 2012 baada ya kuziingilia kingono maiti mbili za wanawake wajawazito huku akisema kuwa amewahi muingilia mwanamke aliyekuwa kapoteza fahamu akidhania alikuwa kafariki. Mwaka huo pia mlinzi wa hospitali moja mjini Memphis, Tennessee US Cameron Wright alikamatwa baada ya kukutwa akifanya ngono na maiti ya mwanawake aliyekuwa ameingizwa mochwari saa chache baada ya kufariki.
 
Anaitwa Williamina McCulloch Dean alizaliwa 2.9.1844 na kunyongwa 12.8.1895 mjini Invercargill kusini mwa New Zealand. ni mwanamke aliyekuwa akijihusisha na kulea, kutunza watoto kwa malipo kidogo. Inaelezwa pia alikuwa anaiba watoto Wlwachanga na kuwauza kwa watu waliokuwa hawana watoto, alikuwa anafanya kazi ya kuwalea watoto wa watu wa chini ya miaka 3 kwa malipo na katika maelezo yake baada ya kukamatwa alisema alikuwa amelea zaidi ya watoto 27. Inaelezwa kuwa watoto 10 kati ya hao walikuwa wazima, watoto 6 walikutwa wamefariki, watoto 4 hawakujulikana kkama waliuliwa au kupotea na 7 waliobaki alikiri kuwauza kwa watu waliokuwa wakihitaji watoto. Polisi nchini humo waliamini kuwa Watoto wengine alikuwa akiwauwa na hiyo ni baada ya kukutwa mashimo mawili aliyozika miili miwili ya watoto katika bustani ya nyumbani kwake. . . Kwasasa tungesema ni kama mtu mwenye kituo cha kulelea watoto wadogo, lakini yeye aliifanya kuwa biashara ya kuiba na kuwauza watoto kwa watu wengine, anaitwa pia Baby Farmer. . . Baada ya Taarifa Hizo Miaka ya 1890's Magazeti Mengi Nchini humo Yaliiandika Taarifa hii Iliyokuwa na Kichwa “A Respectable Married Woman Wants to Adopt a Child; Comfortable home in the Country,”. . Polisi Walifika Nyumbani Kwake Kufanya Uchunguzi na Walikuta kuna Watoto 9 Chini ya Umri wa Miaka 3 Waliokuwa Wanalelewa Huku Kukiwa na Mazingira Machafu, ilielezwa Kuwa Miezi Michache tuu Nyuma Watoto wawili wa Umri wa Miezi 6 Walikufa Hapo. May 2, 1895 Dean Alikutwa Anaingia Katika Treni Akiwa Kabeba Mtoto Mchanga Lakini Wakati Anashuka Hakushuka nae! Inaelezwa Alienda Kumpiga Bei kwa Mtu Waliyekutana humo kwa Treni. Dean Alihukumiwa Kunyongwa, Akanyongwa Augost 12, 1895 na Kuwa Mwanamke Pekee Kuwahi Kunyongwa Katika Historia ya Nchi hiyo, Alizikwa Katika Makaburi ya Winton New Zealand.! . . Mwaka 1893 Serikali Ilitoa Matangazo Katika Vyombo vya Habari Yaliyokuwa na Kichwa:- “Anyone Who took in Kids Under Two for More than Three Consecutive Days with Payment Had to be Registered as a Foster Home and Were Inspected by the Police.”
 
116583023_334038690961085_5779581778392271304_n.jpg
 
Tunafahamu kwamba Uingereza inaongozwa kifalme na kimalkia, na malkia wa sasa wa Uingereza ni Elizabeth II aliyeingia madarakani mwaka 1952, kabla yake alikwepo mfalme George VI ambaye alivyofariki tuu ndipo akaingia Elizabeth. Kabla ya George VI kulikuwepo na mfalme Edward VIII aliyetawala kwa muda wa miezi 12 tuu kati ya January 1936 na December 1936, huyu aliacha ufalme mwenyewe na kuandika historia ya kuwa mtawala wa kwanza wa Uingereza kuachia ufalme kwa hiari yake mwenyewe. Kwanini Aliacha? Kisa ni mapenzi. Ilikuwaje? Edward alikuwa mtoto wa mwisho katika familia, baba yake George V ndiye alikuwa mfalme wa Uingereza, na alikuwa anampenda sana mwanaye huyu hadi kufikia kusema wazi kuwa akifariki yeye basi mwanae huyu wa mwisho ndiye arithi ufalme. Ni kweli baada ya baba yake kufariki January 20, 1936 Edward VIII akaingia madarakani kama mfalme mpya, lakini wakati anaingia alikuwa ameanza kupendana na mwanamke wa kimarekani Wallis Simpson ambaye walikuwa wanajuana tangu miaka mitano nyuma. Edward alitaka kumuoa Wallis, lakini shida ikaja kwa familia na viongozi wengine wa nchi wakisema kuwa Uingereza haiwezi kuwa na malkia kutoka Amerika, kwahivyo Edward hawezi kumuoa mrembo huyo wa kimarekani. Ilifika kipindi Edward alishutumiwa kuwa anataka kumuoa mwanamke wa kimarekani na kumfanya malkia ili kuiangamiza Uingereza, walihofia anaweza kuwa mpelelezi aliyetumwa kuichunguza Uingereza, hii ilipelekea kujihuzuru kwa viongozi wengi wa serikali. Edward aliona isiwe tabu, baada ya kukaa miezi 12 madarakani December 11, 1936 akaamua kutangaza rasmi kuwa anaachia kiti cha ufalme ili awe huru kumuoa mwanamke anaempenda huku akisema kuwa hawezi kuwa mfalme bila yeye, ni kweli aliacha, na Juni 7, 1937 wakaoana. Kaka yake George VI ndiye alichukua kiti cha ufalme ambapo naye baada ya kuariki mwaka 1952 akamuachia ndugu yake Elizabeth II ambaye ndiye malkia hadi sasa. Edward alifariki mwaka 1972 na Wallis alifariki mwaka 1986.
Sawasawa....
 
Kuanzia Mwakani 2021 shirika la anga la Marekani NASA litaanzisha utalii wa nje ya dunia ambapo utaweza kulipia $125,000 na kisha kuanza safari ya masaa 6 hadi nje ya dunia kutalii kwa kutumia usafiri, baloon maalumu. utakaa hadi wiki mbili huko. hii ni zaidi ya milioni 290 za Tanzania. Utalii huu umekuwa ukifanywa tangu miaka iliyopita kwa watu binafasi kulipa mamilioni ya pesa kwenda kutalii huko, lakini haikua rasmi. Tazama Video. Sasa NASA wamepanga kuanzia mwakani 2021 Space Tourism iwe rasmi kabisa kwa gharama ya wastani inayotajwa kuwa kati ya $125,000 hadi $250,000 kwa mtu mmoja kutegemea na muda mtakaokaa huko.
Kabla sijafanya utalii anga za juu lazima kwanza nitimize azma ya kutembelea nchi zisizopungua mia moja Duniani kote.
 
Back
Top Bottom