January 26, 1972 mwanamke wa umri wa miaka 22 Vesna Vulovic raia wa Serbia alinusurika katika ajali mbaya ya ndege ya JAT Yugoslav Flight 367 iliyolipuka angani ikiwa umbali wa futi 33,000 kutoka ardhini. futi 33,000 ni zaidi ya kilomita 10, ilikuwa na abiria 23 na wafanyakazi 5. Siku hiyo ya safari Vesna hakutakiwa kuwepo katika ndege hiyo, alipanda kutokana na makosa ya kuchanganya tiketi, kulikuwa na abiria mwingine aliyekua anaitwa Vesna Nicolic, huyu ndiye alitakiwa kuwemo katika ndege hiyo. Ndege hiyo ilikuwa inatoka Serbia kwenda Denmark, inaelezwa kuwa kundi la magaidi waliweka bomu kwa siri ndani ya ndege hiyo na ndiyo lililopelekea mlipuko huo saa chache baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Belgrade Serbia. Ndege iliripuka angani na kukatika katikati, kipande cha mbela kilianguka chini huku kipande cha nyuma kikianguka pia baada ya dakika tatu, tazama video katika post iliyopita, Picha zaidi zipo Telegram. Vesna alionwa na mwanaume mmoja raia wa Ujerumani aliyekuwa mtu wa kwanza kufika katika eneo la ajali, alimpa huduma ya kwanza hadi pale msaada kamili ulipofika. Baada ya uchunguzi madaktari walipoteza kabisa matumaini ya kwamba Vesna anaweza kupona, alikuwa amevunjika miguu yote miwili, alivunjika uti wa mgongo na pamoja na fuvu, Alikuwa amezimia pia. Baada ya siku tatu hospitalini Vesna alizinduka, kitu cha kwanza kuzungumza alisema anaomba sigara, alikuwa amepooza nusu ya mwili wake kuanzia kiunoni hadi chini. Hakuwa anakumbuka chochote kilichotokea mpaka alipokuja kuambiwa baada ya wiki mbili. "Wengi wanasema kuwa nina bahati, wanakosea, sina bahati, kama ningekuwa nina bahati basi nisingekuwepo katika ajali" Baada ya matibabu ya miezi kadhaa Vesna Alipona kabisa na kuendelea na maisha yake. Alikuja kufariki December 23, 2016 mjini Belgrade Serbia akiwa na umri wa miaka 66.