MWILI wa mrembo Jemima Oresha aliyetumbukia katika maporomoko ya Thompson Falls Nyahururu nchini Kenya _ umeopolewa juzi Jumatano, Agosti 5, 2020 na wakazi eneo la Rwathia kando ya mto ambao waliwajulisha polisi ambao walifika na kuuchukua. Naibu kamishna wa eneo hilo, Patrick Muli amesema mwili huo ulipatikana kilomita chache mbali na eneo alikotumbukia na kwamba Jemima alitembelea Thompson Falls ku-enjoy mandhari ya eneo hilo. Jemima mwenye umri wa miaka 39 alikuwa amesimama kwenye jiwe huku ndugu yake Mangafu akimpiga picha, kwa bahati mbaya alikumbana na mauti. Kikosi kilichowashirikisha maofisa wa KWS, polisi, kitengo cha dharura na wale wa Msalaba Mwekundu kilipinga kambi katika mto huo kuusaka mwili wa marehemu. “Mwili huo ulionekana na wakazi eneo la Rwathia kando ya mto ambao waliwajulisha polisi ambao walifika na kuuchukua,” Muli alisema. Naibu kamishna huyo aliwatahadharisha wakazi na kuwaomba kuwa waangalifu wakati wanavuka mito iliyofurika eneo hilo. Mwathiriwa alisafiri kutoka Kitale kaunti ya Trans Nzoia na alisisitiza kwamba kabla arejee nyumbani angependa kuzuru maeneo hayo yenye mandhari ya kupendeza. Familia yake imekuwa ikipiga kambi eneo hilo ikiitafuta mwili wa mpendwa wao. “Ilikuwa ni tamanio letu kuupata mwili wake ili tumzike mahali ambapo tutakuwa tukiliona kaburi lake,” kakake alisema. Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Nyahururu. **RIP JEMIMA
View attachment 1529889