Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua kuwa ukiwa umechoka huo ndo mda mzuri wa kufanya mazoezi ? Utafiti unaonyesha kuwa mazoezi yana kuongezea nguvu tofauti na watu wanvyofikiria. Mazoezi yanaimarisha afya ya moyo na kusababisha mzunguko wa damu na oxygen uongezeke mwilini na kukuongezea nguvu zaidi. Inapendekezwa kama umechoka ufanye mazoezi magumu kwa mda wa dakika 30 na baada ya hapo utajisikia una nguvu zaidi.
 
Je wajua asilimia 90 ya wachezaji wa mchezo wa boxing au masumbwi hupatwa na magonjwa ya ubongo ? Wengi hupatwa na magonjwa ya Alzheimer's na Parkinson's disease Hii ni kwasababu ya kupigwa kichwani mara kwa mara akiwa anapigana na ngumi za kichwa ndo zinapoint kuliko sehemu zingine za mwili. Hii pia hutokana na ubongo kufunikwa na fuvu na kuna nafasi ndogo sana ya ubongo kucheza.
 
Je wajua kuwa mnyama aina ya Deer/Kulungu anasababisha ajali Milioni 1.5 na vifo 150 kwa mwaka nchini Marekani ? Mnyama huyu husababisha ajali sababu ya kuvuka barabara mara kwa mara. Ajali hizo zinasababisha gharama zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani. Ajali hizi zinatokea wakati asubuhi,kipindi cha baridi na mating season
 
Je wajua ni nani aligundua X-ray? Mwanafizikia wa Ujerumani Wilhelm Conrad Rontgen aliigundua X-ray mwaka 1895. Katikata ulimwengu wa sayansi na teknolojia, ugunduzi huu umetoa mchango mkubwa na waki pekee kwani X-ray ni aina ya kipimo inayotumiwa na watu wengi duniani. Ugunduzi huo ulimpatia tuzo ya Nobel peace prize ya (fizikia) mwaka 1901, na yeye ndo alikuwa mtu wa kwanza kupata tuzo hiyo
 
Je wajua kuwa mtalii wa kwanza kwenda kutalii nje ya sayari (outer space) alitumia kiasi cha dola milioni 20 kwa siku saba tu? Mwaka 2001 Dennis Tito ambaye ni Engineer na Mjasiriamali ndo alikuwa mtu wa kwanza kwenda kutalii nje ya sayari. Alifatiwa na watalii wengine wengi kama yeye kabla safari hizi kusitishwa mwaka 2009, leo hii kampuni kama Space X, Blue Origin na Virgin Galactic zinataka kupelekea watalii kwenda nje ya sayari na kampuni hizi tayari zimeshafanya majaribio ya safari hizi. Ticket moja inaweza kukugharimu Dola Laki 2 hadi 2.5 kwa safari isiyozidi masaa mawili.
 
Je wajua kuwa Album ya "The Marshall Mathers LP" ya msanii wa Hip-Hop Eminem iliuza unit milioni 1.7 ndani ya wiki moja ? "Real slim shady" na "Stan" ni kati ya nyimbo maarufu zinazopendwa sana kwenye album hiyo. Eminem ni mmoja kati ya wasanii bora kuwahi kutokea kwenye Hip-Hop yeye pia ndio msanii pekee kuwa na album mbili (The Marshall Mathers LP & The Eminem show) kwenye album 10 bora za hip-hop zinazoongoza kwa mauzo. Eminem pia ni mmoja ya wasanii wa 5 wa Hip-hop wanaongozwa kwa utajiri mwaka. Akiwa na utajiri wa dola millioni 100 yeye pamoja na Drake wanashika nafasi ya 4 wakiongozwa na Dr Dre, P Diddy na Jay Z. Juzi tarehe 31/08 ametoa album inaitwa Kamikaze na imepata kiki kwani amewashambulia wasanii na watu wengi wametokea kuipenda, Emenim ana studio album kumi kiujumla
 
Je wajua ni nchi gani inapokea wageni wengi kwa ajili ya matibabu ? Nchi zilioendelea zinafaidika kutokana na kupokea wagonjwa kutoka nchi mbali mbali (medical tourism). Malaysia ndiyo nchi inayoongoza duniani na Inapokea wageni zaidi ya 500,000 kila mwaka na mwaka 2016 walizidi wageni zaidi ya 1,000,000. Ubora wa Wataalam na Vifaa vya kutolea huduma ndiyo sababu watu huenda kutafuta matibabu nchi zingine. Malaysia wananufaika zaidi kwa sababu huduma zao zina ubora na ni gharama nafuu ukilanganisha na nchi zingine kama Marekani au Uingereza.
 
Je wajua kuna mwanamichezo mwenye miaka 91 ? Gwiji wa gymnastics Johanna Quaas kutoka Ujerumani alizaliwa mwaka 1925 na alianza kujifunza mchezo huo wa gymnastics mwaka 1934. Sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa akifundisha mchezo huo na baadhi ya wanafunzi wake walichaguluwa kuwakilisha nchi yao kwenye mashindano ya Olympics. Mwaka 1982 alipokua na miaka 57 aliingia kwenye mashindano na kushinda. Alianza kupata umaarufu mwaka 2012 akiwa kwenye mashindano mengine na video yake ilipata watazamaji wengi kwenye mtandao wa youtube akiwa na miaka 86 na kuishikilia record mpaka leo akiwa na miaka 91 kuwa Gymnast mwenye umri mkubwa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…