Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua nimwanamke gani aliyehamasisha harakati za kutokomeza ubaguzi wa rangi na kupigania haki za binaadamu nchi Marekani ? Tarehe 01/12/1955 Mwanadada Rosa Parks (1913-2005) alikamatwa na polisi kwa kosa la kukataa kumpisha na kumpa seat Mmarekani mweupu (mzungu) kwenye basi. Sheria ya Jimbo la Montgomery ncini Marekani ilipiga marufuku watu wenye ngozi nyeusi waliojulikana kwa jina la kibaguzi (negroes), kukaa seat za mbele ambazo zilitengwa kwa ajili ya wazungu. Watu weusi walikaa siti za nyuma, Rosa parks hakuwa amekaa kwenye nafasi walizotengewa wazungu ila Abiria mmoja mzungu aliona kuwa nafasi za kukaa watu weupe ziliisha na akataka watu waliokaa mstari wa kwanza wa zile seat za watu weuzi wanyanyuke ili aweze kukaa. Wawili walikubali wakondoka ila Rosa parks alibaki na kusababisha polisi waingilie kati na kumkamata. Wanaharakati wa haki za binaadamu walitumia kufungwa kwake kama fursa ya kuhamasisha watu kupigania haki za binaadamu kwan habari za tukio lile zilisambaa kwa kasi sana. Iliundwa taasis ya Montgomery Improvement Association na akachaguliwa Reverend Dr. Martin Luther King kuwa rais wa taasis hiyo. Rosa parks anajulikana kama "Mother of the Civil Right Movements"
 
:Mahanandia na mpenzi wake walikutana india wakati mpenzi wake alipoenda kuchukua moja ya kazi yake ya uchoraji ambayo alikuwa akifanya huku akisoma chuo Baada ya siku kadhaa mpenzi wake huyo ambaye anatoka katika familia moja ya kitajiri nchini sweden alivutiwa na kazi yake hiyo na kuvutiwa kimapenzi pia.Kwa bahati mbaya penzi lao halikukaa sana kwa sababu mpenzi wake huyo aliondoka zake kwenda kwao nchini sweden na Mahanandia ambaye kwao walikuwa masikini hakuwa na nauli ya kwenda naye na kipindi hicho alikuwa akisoma chuo katika maswala ya uchoraji Mahanandia alimuahidi kukutana naye tena na na mwakan 1977 aliuza baadhi ya vitu vyake akanunua baiskeli na akamfuata mpenzi wake huyo hadi sweden Familia zao zote zilitia baraka na ndoa ikafungwa wakafanikiwa kupata watoto wawili
 
Je wajua chuo cha kwanza Duniani kinatoka Africa ? Chuo cha University of Timbuktu ni chuo kilichotakana na mafundisho kwenye misikiti mitatu ndani ya mji wa Timbuktu ambako kwa Sasa ni nchi ya Mali ya Afrika magharibi. Katika karne ya 12 uchumi mji wa Timbuktu ulikuwa kwasababu ya biashara zilizokuwa zinafanyika. Bidhaa kama dhahabu, chumvi na viungo mbali mbali. Biashara hizo ziliufanya mji ukuwe na uwe sehemu ya kujifunza kwani ziliwavutiwa watu mbali mbali ikiwemo wasomi na hasa wanazuoni/wasomi wa kiislam. Msikiti wa kwanza wa Timbuktu ulijengwa kipindi mansa kankan mussa aliporudi kutoka safari yake ya kuhiji Mecca Katika ya watu 100,000 walioshi katika mji huo 25,000 walikuwa ni wanafunzi. Quran na mafundisho ya kiislam ndio yalikuwa yanafundishwa na kupewa kipaumbele zaidi lakini masomo mengine yalikuwa yanafundishwa kama, Medicine & surgery, anatomy, botany, evolution, physiology and zoology, astronomy, anthropology, cartography, geodesy, geology, mathematics, physics, chemistry, philosophy, language and linguistics, geography, history pamoja na arts
 
Je wajua chuo cha kwanza Duniani kinatoka Africa ? Chuo cha University of Timbuktu ni chuo kilichotakana na mafundisho kwenye misikiti mitatu ndani ya mji wa Timbuktu ambako kwa Sasa ni nchi ya Mali ya Afrika magharibi. Katika karne ya 12 uchumi mji wa Timbuktu ulikuwa kwasababu ya biashara zilizokuwa zinafanyika. Bidhaa kama dhahabu, chumvi na viungo mbali mbali. Biashara hizo ziliufanya mji ukuwe na uwe sehemu ya kujifunza kwani ziliwavutiwa watu mbali mbali ikiwemo wasomi na hasa wanazuoni/wasomi wa kiislam. Msikiti wa kwanza wa Timbuktu ulijengwa kipindi mansa kankan mussa aliporudi kutoka safari yake ya kuhiji Mecca Katika ya watu 100,000 walioshi katika mji huo 25,000 walikuwa ni wanafunzi. Quran na mafundisho ya kiislam ndio yalikuwa yanafundishwa na kupewa kipaumbele zaidi lakini masomo mengine yalikuwa yanafundishwa kama, Medicine & surgery, anatomy, botany, evolution, physiology and zoology, astronomy, anthropology, cartography, geodesy, geology, mathematics, physics, chemistry, philosophy, language and linguistics, geography, history pamoja na arts
 
Je wajua kuhusu gorofa la Pisa ? Gorofa hili linamunekano tofauti na magorofa mengine kwasababu linaonekana kupinda. Gorofa linapatikana katika mji wa Pisa nchini Italia lina urefu wa mita 56.67 na upande wa pili una mita 55.86, inasemekana watalii takriban milioni 1-5 hutembelea kivutio hicho kila mwaka. Watalii huvutiwa kwa sababu ya huo muonekano wake wakupinda. Lina uzito wa tani 14,500 na kupinda kwa nyuzi 3.99. Lilipo jengwa kanisa kuu (Cathedral of Pisa), ndipo gorofa la Pisa Lilianza kujengwa kama jengo la kuhifadhi kengele kubwa za kanisa hilo. Lilianza kujengwa mwaka 1172 na kumalizika 1372. Kupinda kulianza wakati ujenzi umefikia gorofa la pili kwasababu ya mchanga uliopo kwenye msingi wa gorofa hilo kuhama. Wakandarasi walipumzisha ujenzi kwa miaka 100 sababu ya vita vilivyokumba mji wao kwa mda huo. Walibaini kuwa mda huo ulisaidia sehemu ya msingi kuwa imara na waliporudi waliendela kujenga kufatana na jengo lilivyopinda kuwa upande mmoja mrefu na mwingine mfupi
 
Je wajua kuhusu sokwe aliyeweza kutumia lugha ya ishara ? Koko aliyezaliwa tarehe 4.7.1971 Ni sokwe maarufu duniani kwa sababu ya uwezo wa kutumia lugha ya ishara kuwasiliana na Binaadamu. Koko aliweza kujifunza maneno zaidi ya 1000 kwenye lugha ya ishara na aliweza kuyaelewa maneno ya kingereza zaidi ya 2000. Umaarufu wake ulioneakana hasa alipotokea kwenye majalada ya majarida maarufu duniani kama National Geographic. Koko pia alikuwa anapenda paka (kittens) aliomba kwa ishara kuwa aletewe paka wakukaa nae na walipompa mdoli alionyesha ishara ya kuwa hajafurihishwa na kitendo hicho mpaka walipomletea paka wa kweli. Koko alimpa paka wake huyo jina la All Ball. Koko alizaliwa katika San Fransisco Zoo na alitenganishwa na mama yake akiwa na mwaka mmoja kwa ajili ya matibabu na ndo alipokutana na Francine Patterson amabaye alikuwa anafanya utafiti kwa ajili ya PhD chuo cha Stanford University. Patterson alrirukhusiwa kumtunza Koko kwa miaka minne lakini aliendelea kubaki nae baada ya kujenga naye urafiki. Alianzisha shirika la The Gorilla Foundation ili kumsaidia aweze kuwa mlezi wake. Koko alifariki tarehe 19.6.2018 akiwa na miaka 46.
 
Je wajua kuna takriban tani milioni 100 za taka za plastiki kwenye Bahari za dunia ? Zaidi ya wanyama waishio baharini milioni 1 hufa kwa ajili ya taka za plastiki ?Je wajua kuwa plastic ni miongoni mwa taka zisizo oza? Je wewe unamchango gani kuzuia machafuzi haya ?
 
Je wajua kuna nchi walimu wanalipwa mpaka €100,000 kwa mwaka na zaidi? Nchi ya Luxembourg yenye watu wasiozidi 600,000 ni kati nchi ndogo na pia ni kati ya nchi tajiri duniani. Mwali wa shule ya msingi anaweza kulipwa mpaka €60,000 na mwalimu wa sekondari analipwa takriban €66,000 hadi €90,000 kulingana na uzoefu wake na kwa wale wa ngazi ya juu kabisa mshahara hufika hadi €116,000 sawa na Tshs 293,216,349.63 kwa mwaka
 
Je wajua kuwa watu wasiozidi 1,000 wanaishi mji wa Vatican City ? Mji wa Vatican City unaoyosifika kwa utalii wa kidini, Ina ukubwa wa heka 110 sawa na nusu ya kilomita za mraba. Nchi hiyo imezungukwa kila upande na mji Rome nchini Italia. Vatican City inatambulika Kama nchi na ni Kati ya nchi zilipo katika Umoja wa mataifa ya ulaya (EU). Vatican City inaongozwa na Papa kiongozi wa kidini ya Roman Catholic ambaye kwa sasa ni Papa Francis tokea mwaka 2013. Vatican City ina bendera yake, mwimbo wao taifa, passport zao wenyewe na pia wanatengeneza pesa zao wenyewe. Hawatumii mfumo wa kodi na mapato ya taifa hilo huingia kupitia vivutio vya utalii pamoja na sadaka. Inasemekana zaidi ya watu milioni 10 utembelea Vatican city kila mwaka kuangalia vivutio mbali mbali kama Basilica of St. Peter, Saint Peter's Square the Vatican Museums, the Sistine Chapel na the Raphael rooms. Watu wanaoruhusiwa kuishi katika mji humo ni watu wanoshughulika na dini tu Yani ma Cardinal, Pastor na walinzi waitwao Swiss Guard wenye sare zao maalum. Wafanyakazi 2,400 waningia na kutoka kila siku
 
Je wajua namna ya kumpa huduma ya kwanza mtu aliyepeata mshtuko wa moyo (Cardiac Arrest)? Mtu akipata mshtuko wa moyo, mapigo ya moyo yanasimama na pumzi huwa zinakata kwa mda huo. Hakikisha kwanza kama mgonjwa wako hapumui kisha piga simu Ili update msaada wa ki afya. Ili uweze kumsaidia mtu aliyepeata mshtuko wa moyo itabidi uzingatie ya fuatayo; *Fuatilia muongozo wa picha pia 1. Hakikisha mgonjwa amelalia mgongo kisha upige magoti kando yake na uweke mwisho wa kiganja cha mkono wako katikati ya kifua chake 2. Nyoosha mikono yako kisha uweke kiganja cha mkono wa pili juu ya mkono uliopo kifuani kisha ubane vidole. Hakikisha vidole havigusi kifua na mbavu za mgonjwa 3. Sogea mbele na hakikisha mabega yako yapo usawa wa kifua Cha mgonjwa wako. Kandamiza kifua chake usawa wa inchi 2 kisha achia kifua bila kutoa mikono, rudia kufanaya hivyo mara 30 4. Sogea kwenye kichwa cha mgonjwa wako. Shikilia kichwa na mkono mmoja kisha vuta kidevu chake kufungua kinywa chake kiasi na mkono mwingine 5. Tumia mkono ulioshikilia kichwa kubana pua zake na mwingine shikilia kidevu kisha vuta pumzi na ukutanishe midomo yake na ya kwako alafu pulizia pumzi mdomoni mwake mpaka uone kifua chake kinanyanyuka 6. Kifua cha mgonjwa wako kikishuka achilia mdomo na urudie tokea hatua ya kwanza ya kukandamiza kifua chake mara 30 mpaka utakapo pata msaada wa zaidi wa ki afya
 
Je wajua rekodi ya mbio za mita 1500 katika mashindano ya Commonwealth Games zinashikiliwa na Mtanzania ? Mwaka 1974 katika mashindano ya Commonwealth Games huko Christchurch New Zealand, Filbert Bayi Sanka (67) alivunja rekodi na kuweka rekodi yake kwa kukimbia mita 1500 ndani ya dakika 3 na sekunde 32. Rekodi yake ni kati ya rekodi mbili ambazo hazijawahi kuvunjwa mpaka leo katika mashindano hayo Mafanikio ya Filbert Bayi ni pamoja na kushinda medali ya Silver katika mbio za Olympics za mita 3000 mwaka 1980, Moscow. Alishinda Medali ya Dhahabu katika All-Africa games kwenye mbio za mita 1500 mwaka 1973 Lagos, Nigeria na kutetea ubingwa huo mwaka 1978 Algeirs, Algeria. Filbert Bayi ambaye Sasa ni Secretary General wa TOC (Tanzania Olympics Commitee) ni mwanzilishi wa Filbert Bayi Foundation ilyoanzishwa mwaka (2003) kwa nia ya kukuza vipaji vya michezo kwa watoto nchini na shule za Filbert Bayi kwanzia shule ya awali hadi sekondari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…