Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1594864564628.jpg
 
Ahsante..kwa elimj maridhawa
Je wajua kuwa Abraham Lincoln alikuwa bingwa katika mchezo wa Mieleka (wrestling). Abraham lincoln alikuwa rais wa 16 wa Marekani na Rais wa kwanza kutoka chama cha Republican. Alikuwa ni mwanasheria na mbunge wa jimbo la Illinois kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais. Sababu kubwa ya ushindi wale ilikuwa harakati za kupigania haki za watumwa. Alitumikia kipindi chake kwa miaka minne kwanzia 1861 hadi 1865 alpouwawa. Katika kipindi chake alitokomeza utumwa na kuimarisha umoja wa majimbo wa nchi hiyo Mchezo wa mieleka kipindo hicho ilikuwa ni nani mwenye nguvu zaidi ya mwenzie sababu kulikuwa hamna sheria kama sasa hivi sana sana ilikuwa kama ngumi za mtaani tu. Alikuwa na urefu wa futi 6 ns inchi 4 na mikono mirefu iliyomsaidia kuwa dhibiti wapinzani kwenye mieleka inasemekana kati mapambano zaidi ya 300, alipinduliwa ma mtu mmoja tu, Hank Thompson
 
Je wajua kuwa vita vya Anglo-Zanzibar war vilidumu kwa mda wa dakika 40 tu ? Vita hivyo vilivyotekea 27*08*1896 vilikuwa kati ya uongozi wa Sultan wa Zanzibar na Uingereza. Kabla ya Sultan yeyote kuchukua madaraka, ruhusa ilitakiwa kutoka kwa uongozi wa Uingereza kutokana na Mkataba uliosainiwa na pande hizo mbili mwaka 1886 Alipokufa Sultan Hamad bin Thuwaini mwaka 1896, Sultan Khalid bin Barghash alichukua madaraka kinyume na makubaliano ya mkataba(treaty) huo. Uongozi wa Uingereza ulimuamuru Sultan Khalid aaichie madaraka na aondoke lakini alikataa na kujiwekea ulinzi mkali na kujifungia katika jumba lake(palace) Baada ya kukataa amri hiyo. Uingereza walimshambulia Sultan huyo Saa 3 asubuhi na kuisha Saa 3 na dk 40. Walilipuwa jumba hilo na moto ukawaka kusababisha ulinzi wa sultan huyo kushindwa kujitetea. Baada ya vita hivyo kuisha Sultan Khalid alikimbilia German East Afrika(Tanganyika). Baada ya hapo Uongozi wa Uingereza ulimchagua Sultan mwingine Hamud bin Muhammed anayekubaliana na matakwa yao
 
Je wajua mkia wa mjusi ukikatwa au ukikatika huota na kurudi jinsi ulivyokuwa baada ya miezi 9 ? Mjusi ni miongoni mwa wanyama wachache ambao sehemu za mwili huota baada ya kuondolewa au kukatwa. Watalaam husema mjusi akiwa kwenye hatari au akigundua anawindwa na mnyama huacha mkia wake nyuma huku yeye akikimbia ili vile mkia wake unavyotingishika ubakie kumchanganya mnyama anayemwinda ili atoreke. Baadhi ya wanyama wengine ni kama, Buibui anayeweza kutoshe miguu yake, Deer (kulungu) huweza kutesha mapembe yake tu, starfish (kiti cha pweza) anaweza akaotesha mikono yake hata yakikatwa yote.
 
Je wajua mnyama mwenye mwendo wa taratibu kuliko wote ? Mnyama aitwae Sloth anayeishi nchi za Marekani ya kusini na kati ana mwendo wa taratibu unaomfanya asizidi zaidi ya mita 30 kwa siku moja kwa mwendo wa kilometer 0.004 kwa saa Mwendo huo sio kwa kupenda bali ni kwa sababu ya chakula wanachokula hakina kalori (calories) wala virutubisho vinvyompa mnayama huyo nguvu(energy). Mnyama huyo hula majani magumu yenye sumu kali ambayo haya athiri mwili wao sababu ya mfumo wa kipekee wa kusaga chakula tumboni. Huchukua takbani wili mbili nzima kwa mnyama huyo kumaliza kusaga chakula Hushinda mda mwingi kwenye miti ili kujilinda na wanyama wakali na hushuka chini mara moja tu kwa wiki kwa ajili ya haja kubwa na ndogo. Kucha zao ndefu huwasidia kujivuta na kungangania matawi wakati wa kula na kulala
 
Je wajua kuwa tembo ana hisia kama ilivyo kwa binaadamu? Tembo ndiye mnyama mkubwa kuliko wote wa nchi kavu. Tembo ana uzito wa tani 6 na mda mwingine huzidi zaidi ya hapo na kwa sababu ya uzito huo na mwili wake mkubwa tembo anatakiwa kula kilo 150 ya chakula na liter 220 ya maji kila siku . Tembo wanapatikana bara la Asia na Afrika Tembo huonesha huzuni, furaha na hata mmoja wao akifa huomboleza kama ilivyo kwa binaadamu. Wanaweza kuluwa hisia za tembo mwingine na pia husaidia wale walioumia. Tembo huishi kwenye makundi yanoongozwa na Tembo wa kike mwenye umri mkubwa. Huwaongoza sababu ya uzoefu na kujua wapi wata pata chakula na maji na ni sehemu zipi ni salama au sio salama Kwa sababu ya unangili tembo idadi ya tembo hupungua kila mwaka. Kila siku takriban tembo 100 wanauliwa katika bara la afrika. Tembo 300,000 pekee wamebakia Afrika na 40,000 katika bara la Asia. Pembe zao hutumika kutungeneza bidhaa za ivory na ina thamani sana kwenye mtandao wa biashara haramu duniani. Huwa tuniata pembe lakini kitaalamu zaidi zile ni meno zilizojitokeza
 
Je wajua kuna nchi ambazo wanafunzi husoma elimu ya juu, chuo bure ? Nchi kadhaa zilizoendela huyoa elimu bure kwa wazawa na hata wanafunzi wageni na pia wanatoa huduma hiyo kwa lugha ya kiingereza. Japokuwa elimu ni bure ila hali ya maisha katika nchi hizo ni gharama sana Norway - Vyuo vya serikali vyote vina toa elimu ya chuo bure. Licha ya kuwa na gharama ya maisha kubwa sana pia ni katika ya nchi zinazoongoza kwa baridi duniani Ujerumani - Elimu bure Ujerumani Inatolewa hususan kwasababu wanahitaji wafanyakazi na watumishi wenye uwezo wa hali ya juu (skilled workers) Slovenia - Nchii hii iko karibia na Italy na Croatia sehemu nzuri za kutalii kwa hio ni moja ya sehemu nzuri kwenda kusoma elimi ya juu, Bure Ufaransa - Elimu sio bure nchini humo ila wanafunzi hulipa kidogo sana inategemea na course au program enyewe Finland - Kabla ya mwaka 2017 elimu ilikuwa bure kwa wote ila sasa wanafunzi wageni hulipa ada ya Dola 1650 sawa na Shillingi 3,733,125 au zaidi inategemea na course au program utakayo chukua. Nchi hio pia husaidia na kuwapa scholarship wanafunzi wenye historia ya matokeo mazuri Sweden - Elimu bure ni kwa wale wanaochukua PHd tu. Ila hali ya maisha ni gharama sana na inaweza ikakusumbua
 
Je wajua ni watu wangapi hawajui kusoma na kuandika Tanzania ? 2015 asilimia 80.4 ya watu Tanzania ndio wanaojuwa kusoma na kuandika hivyo idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ni takriban watu 10,780,000 Mtu asiyejua kusoma na kuandika hupata shida ya kujifunza kitu kipya kupitia maandishi, vitabu, magazeti, makala n.k. Pia ni ngumu mtu huyo kujifunza kuhusu haki zake kama binaadamu na wajibu wake katika jamii. Bila kusoma na kuandika ni ngumu mtu kujiendeleza ye mwenyewe hata nafasi za ajira zisizohitaji elimu ya juu pia ni ngumu. Watu wasio jua kusoma na kundika wamenyimwa au wamejinyima uwezo mkubwa sana amabao ni kama tegemezi kwa duniani yetu ya sasa inayoendela kila siku Seychelles-95% Equatorial Guinea-95% South Africa-95% Sao Tome And Principe-92% Libya-91% Namibia-91% Mauritius-91% Cabo Verde-88% Botswana-88% Swaziland-87% Zimbabwe-87%
 
Je wajua kuna mapango yenye mto, misitu na mfumo hali ya hewa ndani yake ? Jina la pango hilo ni "Hang Son Doong" iliyopo Vietnam ndio pango kubwa kuliko yote duniani lenye urefu wa kilomita 5 mwanzo hadi mwisho, urefu kwenda juu ni mita 200 (sawa na viwanja viwili vya mpira) na lina upana wa mita 150 Pango hilo liligunduliwa 1991 na mwenyeweji wa eneo hilo ila watu waliogopa na kushindwa kuingia sababu ya sauti inayosikika kama mwangwi kutokana na mto unavyochurizika pamoja na ugumu wa kufika mpaka kwenye mdomo wa pango hilo Pamoja na uzuri wake watalii wachache hutembelea pango hilo. Watalii wakwanza kabisa waliingia humo mwaka 2013 kwa Dola elfu 3 kila mmoja. Watalii wanaingia humo na vibali ambavyo hutolewa kwa nadra sana, mwaka 2017 vibali 800 tu ndio vilitolewa na nikampuni moja tu ya utalii yenye vibali hivyo. Ndani ya mwaka watalii hurusiwa kuingia kwa msimu unaoza Ferbruary mpaka August sababu baada ua August mvua kubwa hunyesha na kusababisha kina cha maji kuongezeka na kufanya sehemu kubwa ya pango hilo lisiweze kupitika
 
Back
Top Bottom