Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua kuwa mapango ya Amboni caves yaliyopo Tanga yaliumbwa miaka milioni 150 iliopita ? Yana ukubwa wa kilomita za mraba 234. Watafiti wanadai kuwa mapango hayo yalikuwa chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita. Mapango kwa ujumla yapo 10 lakini ni moja ndo linatumika kwa shughuli za kiutalii. Nani anaweza kuongezea chochote kuhusu mapango hayo kama kweli tunapenda utalii wa ndani?
 
Je wajua kuwa the great pyramid ya misri ina umri wa miaka 3000 ? Jengo hili ndo la kwanza kujengwa kati ya pyramids 3 za misri (pyramids of giza) jengo hili maarufu lina urefu wa futi 479 na ni moja kati ya maajabu saba ya dunia. Mpaka leo wanasayansi hawajui ni jinsi gani waliweza kujenga pyramids hiyo kutumia mawe zaidi ya milioni 2 na yenye uzito wa tani 2 mpaka 60. Pyramids hizi hupokea wageni zaidi ya milioni 5 kwa mwaka.
 
Je wajua kuna pochi yenye thamani ya dola milioni 3.8 (8,642,720,000 Tshs) ? Pochi hiyo inayojulikana kama Mouawad 1001 Nights Diamond Purse imetengenezwa kutumia karat 18 za Dhahabu pamoja na Almasi 4,517 kuifanya kuwa pochi yenye bei ghali zaidi duniani. Pochi hii imetengenezwa na House of Mouwad ambao ni magwiji wa kutengeneza bidhaa za thamani kama cheni, hereni pete n.k. kutumia madini ya thamani.
 
Je wajua ni ufalme gani uliodumu kuliko yote duniani ? Ufalme wa Japani ulianzishwa mwaka 660 BC na mfalme Jimmu, mfalme wa kwanza wa japan. Nchini Japan Mfalme (Akihito tokea mwaka 01*7*1989) ndio anayemteua waziri mkuu ambaye ndio mkuu wa shughuli za kisiasa nchini. Mfalme akihito anasemekana kuwa mfalme wa 125 nchini humo. Mrithi wa ufalme huo ni mwanae wa kwanza wa kiume, Prince Naruhito
 
Je wajua kuna mji uliojengwa juu ya mlima ? Machu Picchu ni mji uliojengwa mwaka 1450 juu ya milima ya Andes (the andes) nchini Peru. Inasemekana mji huo ulijengwa kwa ajili ya mfalme wa jamii hiyo ijulikanayo kama the Incas. Mji huo ulitelekezwa baada ya miaka 80 sababu ya wakoloni kutoka Spain kuvamia nchi hiyo. Wakoloni hao hawkufanikiwa kuugundua mji huo mpaka mwanahistoria wa marekani Hiram Bingham kuugundua mwaka 1911. Mwaka 2007 sehemu hiyo ilitambulika kuwa miongoni mwa maajabu 7 ya dunia. Wanasayansi hushangazwa hasa na ufundi ulitumika kujenga mji huo sababu majengo hayo yalijengwa kwa kuunganisha mawe bila kutumia vifaa ambavyo vinatumika sasa (dry stone walling).
 
Je wajua jinsi ya kuacha kuvuta sigara ? Sigara inasababisha vifo vya watu milioni 6 kila mwaka na inajulikana ka ambao hawavuti na wanaovuta pia kuwa ina madhara makubwa sana. Licha ya kuuwa mapafu na kisababisha cancer ya mapafu, sigara ina madhara kwenye kila kiuongo cha mwili wa Binaadamu Kemikali iliyopo ndani ya sigara (nicotine) ndio inayosababisha mtu awe mlevi wa sigara Nicotine husababisha mwili uzidishe uzalishaji wa chemicali kwenye ubongo iitwayo dopamine ambayo hukupa hisia ya kuburudika au kuridhika na kitu flani. Dopamine huzalishwa hata mtu akitumua madawa ya kulevya au kilevi chochote alichozoea kutumia Ni ngumu kuacha kwa haraka haraka au kwa kushtukiza na mara nyingi mtu akishindwa hukata tamaa na kurudia kuvuta tena sigara Andaa au panga siku ambayo itakuwa siku yako ya mwisho kuvuta sigara. Kabla ya siku hio haijafika unatakiwa uwe umepunguza au kuacha kabisa. Ifikapo siku hiyo usivute kabisa sigara na jitahidi usiwe unafikra kuhusu sigara kwa siku hiyo Tumia dawa ambazo zinasaidia kupunguza kilevi cha nicotine NRTs. Dawa hizi zina idadi ndogo ya nicotine. Zinasaidia kumfanya mtu aache kuizoea taratibu kemikali hiyo kama kilevi. Kusudio lake kubwa ni wewe kuipata ile nicotine bila madhara ya makemikali mengine yaliopo kwenye sigara Kwa "ushauri wa daktari" tumia dawa za ambazo zinaiwa au zinaondoa ile hamu ya nicotine mwilini (Bupropion na Varenicline). Dawa hizo hudhibiti jinsi ubongo unavyozoea nicotine hivyo hueza kuleta madhara kama kushikwa na hasira kuwa na huzuni Unaweza ukapata pia ushauri kwa watu hasa waliofanikiwa kuacha kuvuta sigara pia na jitahidi kuepuka vitu au tabia ambayo hufanya utake kuvuta sigara mfano watu hupendelea kuvuta pinda wanapomaliza kula au kabla na baada ya kufanya kitu fulani
 
Je wajua ni mwanamichezo gani anongoza kwa kutoa misaada duniani ? Wanamichezo hujulikana kuwa na utajiri mwingi sana na baadhi yao hukumbuka walipotoka na kutoa misaada pale wanapo weza Cristiano Ronaldo anajulikana hasa kwa kuwa mmoja ya mcheza soccer bora aliyewahi kutokea duniani na pia anajulikana kuwa ndiye mwanamichezo tajiri kuliko wote duniani, ukiacha wengine waliostaafu na watu wengi hawajui kuwa yeye ndiye mwanamichezo anayeeongoza kuliko wote kutoa misaada hana tattoo mwilini mwake sababu anachangia damu mara kwa mara Ni balozi wa mashirika ya msaada makubwa duniani kama Save the Children, Unicef na World Vision. Alipochaguliwa kwenye kikosi bora cha mwaka na shirika la soka barani ulaya Uefa alilipwa €100,000 na alitoa zitoa kama msaada kwenye shirika la red cross Alitoa €600,000 alizopata kama bonus za kushinda kombe la Club Bingwa Ulaya kama msaada Pia alitoa $165,000 kwenye kitengo cha cancer katika hospitali iliyomtibu mama ake Aliposhinda kiatu cha mfungaji bora ligu kuu ya Spain alikiuza kwa mnada na alifanikiwa kukuza £1,200,000. Hela hizo zilitumima kujenga shule Gaza, sehemu iliyoathiriwa na vita *Hizi ni baadhi tu ya misaada alitoa mwanamichezo huyo*
 
Je wajua kuwa kupigana inaruhusiwa kwenye mchezo wa Ice Hockey ? Mchezo wa Ice Hockey sio maarafu sana duniani kote ila kwa nchi kama Canada na nchi zingine barani ulaya zenye baridi hasa baridi kali wakati msimu wa baridi (Winter). Kupigana ni mmoja ya sheria katika mchezo huo na wanatwangana hadi mmoja atakapo anguka kwenye barafu ndo muamuzi anaruhusiwa kuamilia na kuwazuia Mjadala unaendela kila siku kuhusu sheria hii kwani inaweza kuleta madhara makubwa kwa wachezaji. Mchezo huo unachezwa na watu sita kila timu, mlinda mlango mmoja na wachezaji wa ndani watano ambao hutumia fimbo kupigania kukipiga kimpira kidogo cheusi ili kila mmoja aweze kukiingiza kwenye goli la mwenzie. Wachezaji huvaa viatu vya kipekee vinavyo fanya waweze kuteleza kwenye barafu hiyo.
 
Screenshot_20200812-145911.png

AllezParis
 
Je wajua kuwa vita vya Anglo-Zanzibar war vilidumu kwa mda wa dakika 40 tu ? Vita hivyo vilivyotekea 27*08*1896 vilikuwa kati ya uongozi wa Sultan wa Zanzibar na Uingereza. Kabla ya Sultan yeyote kuchukua madaraka, ruhusa ilitakiwa kutoka kwa uongozi wa Uingereza kutokana na Mkataba uliosainiwa na pande hizo mbili mwaka 1886 Alipokufa Sultan Hamad bin Thuwaini mwaka 1896, Sultan Khalid bin Barghash alichukua madaraka kinyume na makubaliano ya mkataba(treaty) huo. Uongozi wa Uingereza ulimuamuru Sultan Khalid aaichie madaraka na aondoke lakini alikataa na kujiwekea ulinzi mkali na kujifungia katika jumba lake(palace) Baada ya kukataa amri hiyo. Uingereza walimshambulia Sultan huyo Saa 3 asubuhi na kuisha Saa 3 na dk 40. Walilipuwa jumba hilo na moto ukawaka kusababisha ulinzi wa sultan huyo kushindwa kujitetea. Baada ya vita hivyo kuisha Sultan Khalid alikimbilia German East Afrika(Tanganyika). Baada ya hapo Uongozi wa Uingereza ulimchagua Sultan mwingine Hamud bin Muhammed anayekubaliana na matakwa yao
😁dk 40?
 
Back
Top Bottom