Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua kuna nyumba yenye thamani ya Dola bilioni 1 ? Bilionea Mukesh Ambani kutoka india ndiyo anamiliki nyumba yenye thamani au bei ghali kuliko zote duniani. Antilia ndio jina la nyumba yake iliyopo Mumbai, India na anaishi yeye na familia yake, mke na watoto wa 3. Bilionea huyo mwenye Dola Bilioni 43.2 ndio tajiri namba moja India na tajiri wa 18 dunia nzima. Jumba hilo lilichukua miaka 4 kutengenez na lina ghorofa 27 na ina nafasi ya kuishi ya mita za mraba 400,000 na ina ina urefu wa futi 550. Alitaka kuijenga jumba kubwa na la kipekee kwa hivyo hamna floor (ghorofa) zinafonana
 
Je wajua ticket ya ndege yenye bei ghali zaidi duniani ? "The residence" kutoka kampuni ya ndefe ya Etihad Airways ni huduma inayokupa chumba chako mwenye binafsi ndani ya ndege chenye sebule choo na bafu. Kutoka New York, Marekani hadi Abu dhabi, Falme za kiarabu (United Arab Emirates) huduma hiyo itakugaharimu Dola 64,000. The Residence ina toa huduma zinazofana na hotel yenye hadhi ya nyota tano Wateja hupata huduma ya kuletwa airport na gari ya kifahari aina ya limousine na pamoja na muhudumu wako binafsi atakaye shughulikia kila kitu kuhusu safari yako hivyo hamna haja ya kupanga foleni ili ukaguliwe. Pia utakuwa na sehemu yako binafsi ya kusubiria ndege (private lounge) na humo ndani pia unaweza kupata huduma kama massage na spa kama mda unaruhusu. Utasindikizwa hadi ndani ya ndege hadi kwenye chumba chako (private cabin) ambacho kimegawanya sehemu tatu, sehemu ya kukaa, kulala(kitanda) na bafu. Ndani ya ndege pia utakuwa na muhudumu wako binafsi (butler) atakaye kuhudumia kwa safari yako nzima. Atakuletea chakula, vinywaji, kukuandalia bafu na hata ukitaka company ya kuongea Ukitaka kuitizama video ya the residence flight from abu dhabu to mumbai .....
 
Je wajua kuwa kuna chumba cha hoteli unaweza kulipia hadi Dola 80,000 (180,672,000 Tshs) kwa siku moja ? The Royal Penthouse Suite ya Hotel President Wilson ndio chumba cha hotel chenye gharama zaidi dunia nzima. Ndani yake kuna vyumba 12 na vyoo 12 vilivyotengenezwa na marumaru. Licha ya kuwa na bei kubwa pia ni chumba cha hotel kikubwa kuliko vyote barani Ulaya ikiwa na mita za mraba 1680 Miongoni mwa wateja waliwahi kulipia chumba hiko ni Bill Clinton na Bill Gates. Kwa sababu kinaweza kuchukua wageni 12 unaweza ukaigawa bei hiyo na kikundi au marafiki zako na beu itakuwa Dola 6,600 kwa kila mmoja au unaweza kulipia chote mwenyewe. Kati vyumba hivyo 12, 2 ni master bedroom vyenye mabafu yenye jacuzi inayotazamia ziwani na ndani mabafu hayo zimejaa bidhaa kutoka kampuni maarufu ya mitindo ya Hermès Miongoni mwa vivutio ndani ya hoteli hiyo ni terrace au balcony unayoweza kupata picha nzuri ya ziwa la Lac leman pamoja na darubini (telescope) ya kuangalia nyota wakati wa usiku. Ndani ya chumba hicho unweza ukaangalia Tv yenye screen kubwa kuliko duniani. Chumba hicho huwa kina sifa ya kuwa na wageni maarufu kama wanasiasa na wasani ambao wanasafiri na msafara wa watu kwahiyo kuna ulinzi wa hali ya juu. Vioo vya vyumba hivyo ni bullet proof yani hazipenyezi risasi. Pia kuna lifti binafsi kwa wageni wa chumba hicho. Chumba hicho pia kina gym ya mazoezi ndani yake.
 
Je wajua unapoteza lita ngapi ya maji kila siku. Mwili wa binaadamu unapoteza lita 2 hadi 3 za maji kila siku na inashauriwa unywe lita hizo hizo za maji kila siku kwani kuna mahdara makubwa ya kuto kunywa maji kutosha katika mwili wako Kabla sijaorodhesha sababu muhimu za kunywa maji ni vyema kutambua kuwa takribani watu bilioni 2.1 wanashindwa kunywa maji yaliyo safi na salama ambayo ni hatari sana kwa afya Njia kubwa ambayo binaadamu hupoteza maji kupitia mkojo. Mkojo hupoteza lita 1.5 za maji mwilini. Kutokunywa maji inasabisha figo kufanya kazi kupita kiasi kuchuja maji na dalili yake kubwa ni mkojo kuwa wa njano. Mwisho wa siku figo huchoka na kufeki kutokana na idadi ndogo ya maji mwilini Njia nyingine ni kupitia jasho. Wafanya mazoezi hushauriwa kunywa maji kabla na baada ya kufanya mazoezi. Maji pia huimarisha afya ya ngozi na kuwa na ngozi nyororo. Maji pia hutoka mwilini kupitia mvuke kwa njia ya kupumua. Binaadamu tunapumua mda wote na maji hutoka kupitia mvuke. Binaadamu hupoteza mililita 300 hadi 500 za maji kila siku kwa kupumua. Maji huasidia kulainisha kamasi kwenye njia za hewa kusadia hewa kupita bila kipingamizi
 
Je wajua faida za kula matunda kila siku ? Kila mtu hula matunda na wengi hula sababu matunda kwa kawaida yana ladha nzuri. Ila kwa wala wanao kula matunda kama sehemu ya chakula chao cha kila siku, hupata faida sana kwani matunda yana virutubisho muhimu vinavyosaidia kudumisha afya ya mwili. Matunda hujulikana kama chakula bora zaidi sababu ya uhaba wa vitu kana mafura, kalori na sodium. Matunda yana virutubisho muhimu ambavyo binaadamu huvikosa sababu yakutokula matunda kama Vitamin C, folic acid, dietary fiber na potassium Potasium iliyopo kwenye matunda husadia kutuliza shinikizo la damu isizidi au kupungua kiasi chake. Matunda yenye pottasium ni kama Ndizi, Prunes, Peach, Apricot na Orange Juice Folic acis husaidia mwili kutengeneza seli nyekundu za damu (red blood cells). Inashauriwa kwa wanawake wanotarajia kupata watoto wapate kirutubisho hicho kwa wingi pamoja na kukipata kupitia vyakula vingine vyenye kirutibisho hiko Virutubisho vya fiber vilivyopo kwenye matunda husaidia kupunguza cholesterol kwenye damu ili kuzuia magonjwa ya moyo. Fiber husaidia mtu kushiba bila kuingiza kalori (calories) nyingi mwilini. Fiber hiyo hupatikana matunda yakiliwa mazima na siyo kwa njia ya juisi Vitamin C husaidia kukuza na kutibu tissue zote katika mwili wa binaadamu, husadia kuponya sehemu zenye uwazi na vidonda pia husaidia kuimairisha afya ya meno na fizi
 
Je wajua ni nani anayeshikilia rekodi ya kushinda mashindano ya Grand Prix ya Formulae 1 ? Michael Schumacher kutoka Ujeramani anaongoza kwa kuwa bingwa mara 91 katika mashindano hayo ya mbio za magari. Mashindano hayo hufanyika sehemu mbali mbali dunia nzima kila mwaka. Shindano lake la kwanza lilikuwa ni Belgian Grand prix 1992 na la mwisho lilikuwa ni Chinese Grand Prix 2006. Amestaafu mchezo huo mwaka 2006 na kurudi tena mwaka 2010 na alipoona matokeo yake sio mazuri alistaafu kwa mara ya pili 2012. Kutokana na mchezo huo Schumacher ana utajiri wa dola milioni 800.
 
Je wajua ni mwaka gani nchi nyingi za ki Afrika zilipata uhuru. Mwaka 1960 unajulikana kama the year of independence kutokana nchi 17 za ki Afrika kupata uhuru huku nchi 14 kati ya hizo zilitawaliwa na Ufaransa Harakati za kutafuta uhuru zilipamba moto baada vita vya dunia vya pili kuisha. Wa Afrika katika nchi hizo walianza kuwadai wakoloni ahadi walizowapa katika kuwasidia kwenye vita hivyo. Madai ya wa Afrika pamoja na msaada kutoka marekani,wakoloni hao walilazimika kuwapatia uhuru nchi hizo ambazo ni Cameroon - 01*01 Togo - 04*27 Madagascar - 06*26 Democratic Rebulplic of Congo - 06*30 Somalia - 07*01 Benin - 08*01 Niger - 08*03 Burkina Faso - 08*05 Ivory Coast - 08*07 Chad - 08*11 Central African Republic - 08*13. The Republic of Congo - 08*15 Gabon - 08*17. Senegal - 08*20, Mali - 09*22. Nigeria - 10*01 Mauritania - 11*28
 
Je wajua ni mnayama gani mkubwa kuliko wote duniani ? Nyangumi ni wanyama wakubwa waiishio baharini Kwa ambao hawajui nyangumi sio aina ya samaki ! Nyagumi anazaa kama binaadamu na mamalia wengine ila yeye hanyonyeshi na pia akikaa mda mrefu kwenye maji anaweza kuzama kwahiyo lazima aibuke apate kupumua kutumia tundu juu ya mgongo wake Aina ya nyangumi aitwae "Blue whale" ndiye mnyama mkubwa zaidi duniani mwenye urefu na upana wa mita 29.9 (futi 98) na uzito tani 181 na pia anajulikana kuwa mnyama mkubwa kuliko wote waliowahi kuishi duniani
 
Daxing International Airport ndio terminal kubwa ya Airport kuliko zote duniani, ipo mjini Beijing, China imejegwa kwa miaka mitano inaukubwa wa 700,000 Square Meters kama wastani wa Viwanja 98 vya mpira wa miguu, bajeti yake imetumika kama dole billion moja sawa na hela ya madafu 2,280,000,000,000 🥴
 
Je wajua kuna mnyama analala jicho moja wazi ? Mnyama aina dolphin ni mmoja ya aina ya mamalia wanaoishi baharini wakiwemo na nyangumi. Wakati wa kulala inasemekana upande mmoja wa akili yake umelala na mwingine bado unafanya kazi (conscious) kumfanya alale huku jicho moja kaacha wazi.Anafanya hivi ili ajilinde akiwa analala na wanyama hatari wa baharini kama Papa. Pia kwa vile yeye ni mamalia akilala usingizi wa moja kwa moja atazama hivo lazima aibuke kupumua alafu arudi tena kulala au hulala kwenye kina kifupi cha maji.
 
Je wajua kuna aina ya mbuzi wenye uwezo wa kupanda ukuta? Mbuzi pori aina ya Alpine Ibex huishi sehemu za milimani kwahio mda mwingi wamezoea kupanda kina kirefu kutafuta majani ya kula. Kwenye ukuta wa bwawa la maji wenye urefu wa mita 30 au Futi mia Huko nchini Italia wameonekana wakipanda ukuta ili kulamba chumvi iliyopo kwenye ukuta huo
 
Screenshot_2020-08-12 Instagram.png
 
Je wajua ni mnyama gani ana hisia kali zadi ya harufu kuliko wote? Bears au Dubu ndo mnyama mwenye hisia kali zaidi ya harufu ana weza akasikia harufu ya mzoga uliopo zaidi ya kilometer 30. Wanyama hawa hula nyama, matunda na baadhi ya mimea au majani (Omnivores). Binaadamu anazidiwa na mbwa kusikia harufu zaidi ya mara 100 na aina ya mbwa anayejulikana kama blood hound anauwezo mara 300 zaidi ya binaadamu amabaye ni mbwa mzuri kwa ajili shughuli za Uwindaji. Bear anauwezo mara 2,100 zaidi ya binaadamu. Uwezo huo unawasaidia wanyama hawa kutafuta chakula akiwa ana winda, kuepusha hatari hasa wakiwa na watoto
 
Je wajua ni mnayama gani mkubwa kuliko wote duniani ? Nyangumi ni wanyama wakubwa waiishio baharini Kwa ambao hawajui nyangumi sio aina ya samaki ! Nyagumi anazaa kama binaadamu na mamalia wengine ila yeye hanyonyeshi na pia akikaa mda mrefu kwenye maji anaweza kuzama kwahiyo lazima aibuke apate kupumua kutumia tundu juu ya mgongo wake Aina ya nyangumi aitwae "Blue whale" ndiye mnyama mkubwa zaidi duniani mwenye urefu na upana wa mita 29.9 (futi 98) na uzito tani 181 na pia anajulikana kuwa mnyama mkubwa kuliko wote waliowahi kuishi duniani
Kimshinda tembo
 
Je wajua kuna mtu aliwahi kuhitimu Chuo akiwa na miaka 10 ? Michael Kevin Kearney amabaye sasa ana umri wa miaka 34, alipata shahada ya anthropologia katika University of Sourthen Alabama mwaka 1994 akiwa na miaka 10 na kuweka record mpaka leo kuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo zaidi kupata shahada na kuhitimu chuo. Michael pia aliweka record ya kuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo pia kupata shada ya uzamili akiwa na miaka 14 katika chuo cha Middle Tennesse State University na record hiyo ilivunjwa mwaka 1999. Alianza kufundisha chuo akiwa na miaka 16 na alipofikisha miaka 18 alipata shada ya nyingine ya uzamili ya Computer Science. Alipata PhD akiwa na umri wa miaka 22 na akaendelea na kazi ya kufundisha Chuo Middle State Tennesse University
 
Je wajua kuna shule yenye wanafunzi 55,000? (Eneo la msasani Kinindoni Dar es salaam wanaishi watu 48,920). City Montessori School (CMS) iliyopo India ndio shule yenye wanafunzi wengi kuliko shule zote duniani na ina wafanyakazi 4,500. Shule ilianzishwa na Dr Jagdish Gandhi and Dr Bharti Gandhi kwa mtaji wa Rupee 300 walizochukua kwa mkopo. Shule ilianzishwa mwaka 1959 ikiwa na wanafunzi wa 5.
 
Back
Top Bottom