Je wajua faida za kula matunda kila siku ? Kila mtu hula matunda na wengi hula sababu matunda kwa kawaida yana ladha nzuri. Ila kwa wala wanao kula matunda kama sehemu ya chakula chao cha kila siku, hupata faida sana kwani matunda yana virutubisho muhimu vinavyosaidia kudumisha afya ya mwili. Matunda hujulikana kama chakula bora zaidi sababu ya uhaba wa vitu kana mafura, kalori na sodium. Matunda yana virutubisho muhimu ambavyo binaadamu huvikosa sababu yakutokula matunda kama Vitamin C, folic acid, dietary fiber na potassium Potasium iliyopo kwenye matunda husadia kutuliza shinikizo la damu isizidi au kupungua kiasi chake. Matunda yenye pottasium ni kama Ndizi, Prunes, Peach, Apricot na Orange Juice Folic acis husaidia mwili kutengeneza seli nyekundu za damu (red blood cells). Inashauriwa kwa wanawake wanotarajia kupata watoto wapate kirutubisho hicho kwa wingi pamoja na kukipata kupitia vyakula vingine vyenye kirutibisho hiko Virutubisho vya fiber vilivyopo kwenye matunda husaidia kupunguza cholesterol kwenye damu ili kuzuia magonjwa ya moyo. Fiber husaidia mtu kushiba bila kuingiza kalori (calories) nyingi mwilini. Fiber hiyo hupatikana matunda yakiliwa mazima na siyo kwa njia ya juisi Vitamin C husaidia kukuza na kutibu tissue zote katika mwili wa binaadamu, husadia kuponya sehemu zenye uwazi na vidonda pia husaidia kuimairisha afya ya meno na fizi